Serikali imeihakikishia Timu ya Waangalizi ya Uchaguzi ya Wabunge-Wanawake kutoka Jumuiya ya Madola (CWP) kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025 utakuwa huru, haki na wazi. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi alipokutana na timu hiyo jijini Dodoma Oktoba 28, 2025. Mhe. Chumi alisema Serikali kupitia taasisi husika zikiwemo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imekamilisha maandalizi yote muhimu kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia Katiba ya Nchi, sheria za uchaguzi na vigezo vya kidemokrasia. Alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa aina yake kutokana na kuwa jumuishi zaidi ambapo wagombea 17 wa nafasi ya Rais, watatu ni wanawake na 10 ni wagombea mwenza, huku ikishuhudiwa pia kuwa idadi kubwa ya wanawake wanawania nafasi za ubunge na udiwani katika pande zote za muungano. Naye, Kiongozi wa timu hiyo, Mhe. Ndan...