Posts

RAIS SAMIA AZINDUA RASMI KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA BWAWA LA JULIUS NYERERE.*

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 leo, tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, mkoani Pwani. Viongozi mbalimbali wameungana na Rais Samia katika uzinduzi huo, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Moustafa Madbouly; Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi; pamoja na viongozi wengine. Uzinduzi wa JNHPP ni kilele cha utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati uliotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huo umegharimu takribani shilingi trilioni 7.452, sawa na dola za Marekani bilioni 3.35. Ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025. JNHPP imeongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini na kuimarisha usalama wa nishati. Kwa sasa, u...

RAIS SAMIA AWASILI JNHPP

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi na viongozi wengine wakati alipowasili katika eneo la Mradi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP). Rais Samia atazindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 leo tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA ENEO LA HAFLA YA UZINDUZI WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (JNHPP)

Image
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kumiminika katika eneo la hafla ya uzinduzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), wakishuhudia tukio hilo muhimu katika historia ya maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Hafla hiyo inafanyika leo, huku wananchi na wageni mbalimbali wakifika katika eneo la tukio kushiriki katika tukio hilo kubwa linalohusisha uzinduzi rasmi wa mradi huo wa kimkakati wa kuzalisha umeme. Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuzindua rasmi Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuzungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali watakaoshiriki katika hafla hiyo.

WAZIRI KOMBO APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KWA BALOZI MTEULE WA UBELGIJI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati  za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ubelgiji nchini Mhe. Lot Debruyne, katika Ofisi ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam.  Baada ya tukio hilo viongozi hao walijadili namna bora ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji. Akizungumza na Balozi Mteule wa Ubelgiji Mhe. Waziri Kombo alisisitiza azma ya kuhamisha ushirikiano kutoka kwenye misaada na kuelekea katika kufanya biashara na uwekezaji. Mhe. Waziri Kombo ameeleza juu ya fursa za ushirikiano katika kilimo na umwagiliaji, uhamishaji wa maarifa na ujuzi, pamoja na mitambo na teknolojia za kisasa za kilimo.  Pia alihimiza kuongezwa kwa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji akitaja ongezeko la watalii kupitia safari za moja kwa moja za Shirika la Ndele la Ubelgiji (Brussels Airlines) kwenda Kilimanjaro na Zanzibar kama fursa ya...

PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

Image
Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari na maelekezo yanayotolewa na wataalamu na mamlaka husika ili kupunguza madhara yanayotokana na majanga na maafa. Prof. Kabudi ametoa wito huo tarehe 19 Agosti, 2026 wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. “Ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga, huku akiwataka kuendelea kufuata taarifa na maelekezo rasmi kutoka kwa wataalamu na mamlaka zinazohusika na masuala ya maafa.” Katika hatua nyingine, alisema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema na kujenga ustahimilivu wa jamii ili kuongeza uwezo wa wananchi kukabiliana na majanga na kupunguza madhara yanayotokana na matukio hayo. Alisema uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga kwa ufanisi unategemea uwepo wa mifumo madhubuti,...

Serikali yasisitiza ushirikiano na Sekta Binafsi ( PPP)

Image
Serikali yasisitiza ushirikiano na Sekta Binafsi ( PPP) Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuongeza uwekezaji na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Maji katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2024 hadi 2025. Waziri Aweso amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi, sambamba na kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za maji nchini. Amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji vijijini, kwasababu Serikali inalenga kumaliza uhaba wa maji katika vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya huduma ya maji. Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuzielekeza ka...

ZAIDI YA WATU 20 WAHOJIWA SAME KWA TUHUMA ZA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI

Image
ZAIDI YA WATU 20 WAHOJIWA SAME KWA TUHUMA ZA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI Na Musa Mathias,  Same, Kilimanjaro.  Tafadhali Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa Zaidi ya watu 20 wanahojiwa na Jeshi la Polisi wilayani Same kwa tuhuma za kudaiwa kuendesha shughuli za uchimbaji haramu wa madini katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kinyume cha sheria na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira. Akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amesema Kamati ya Usalama ya wilaya ilipata taarifa za siri kuhusu uchimbaji huo katika maeneo mbalimbali na kufika kujiridhisha, ambapo ilibaini kuwepo kwa shughuli hizo. Amesema baada ya kubaini hali hiyo, Kamati iliunda timu ya kwanza ya wataalamu kutoka RUWASA, Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Maafisa Mazingira na Maafisa Madini, iliyofanya uchunguzi katika maeneo yote na kubaini uchimbaji haramu katika kata saba pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira. Aidha, iliundwa timu ya pili kutoka ndani ya Kama...