CCM YABADILISHA MAISHA NAMONGE


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imebadilisha maisha ya watu wa Kata ya Namonge  kwa kuleta miradi ya maendeleo ikiwemo kufungua barabara, maji na umeme.

Dkt. Biteko amesema hayo Oktoba 1, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Bwenda, Kata ya Namonge wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Dkt. Biteko amesema kuwa awali Kata hiyo haikuwa na maji, umeme,barabara na hata walimu waliochaguliwa kufundisha katika shule za Kata hiyo hawakufurahia kazi zao kutokana na hali iliyokuwa.

“Kituo cha afya kimekamilika, gari la kubeba wagonjwa kesho litakuwepo, leo tuna shule 14 za msingi, shule tatu za sekondari na tutataka kujenga shule zingine za kidato cha tano na sita,” amesema Dkt. Biteko.


Ameendelea kusema ikiwa wananchi hao wanahitaji maendeleo zaidi amewaomba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kupiga kura huku akiwahimiza kuchagua viongozi wa CCM.

Amesema CCM ina mpango wa kukarabati Shule ya Bwenda, kupeleka umeme maeneo yote ambayo hayana umeme.

Pia, amewahimiza wananchi wa Kata hiyo kumpigia kura mgombea udiwani Mlalu ambaye mara zote ameyapa kipaumbele maendeleo ya wananchi.

“ Kura 31, 772 za wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika Kata hii zimchague mgombea wetu wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zinichague Mbunge Biteko na Diwani Mlalu kisha mtudai maendeleo,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Pia amewaeleza wananchi hao kuwa Oktoba 12, Dkt. Samia atatembelea Jimbo lao hivyo wajitokeze kwa wingi ili kuashiria upendo na shukrani zao kwake.


Naye, Mgombea wa Udiwani Kata ya Namonge, Malalu Bundala amesema kuwa miradi yote iliyopo kwenye Kata hiyo imegharamiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ametolea mfano wa miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika kijiji cha Nyamagana na Shule Shikizi Bwenda.

Kuhusu miradi ya maji amesema Kata hiyo imepata visima viwili ikiwa ni hatua ya Rais Samia ya kutatua changamoto ya maji na kusogeza karibu zaidi huduma huyo kwa wananchi kwa kuchimba visima vitano katika kila jimbo.

Pamoja na hayo amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuwachagua wagombea wote wa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO