RAHA YA UHIFADHI NI KUISHI VIZURI NA MAJIRANI


Na mwandishi wetu 

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro anayesimamia Uhifadhi,Utalii na Maendeleo ya Jamii   Joas Makwati Oktoba 1 mwaka 2025 ameongoza kikao cha ujirani mwema na viongozi wa maeneo  ya vijiji vya jirani na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano ili kujenga mazingira mazuri ya kufanya kazi pamoja.

Katika kikao hicho pamoja na watendaji wengine Naibu Kamishna aliongozana na Kamishna Msaidizi Mwandamizi  anayeshughulikia maendeleo ya jamii Bi. Gloria Bideberi ambapo viongozi wote walikubaliana  kufanya kazi kwa pamoja.

Viongozi wa vijiji  wa wilaya ya Karatu na Monduli walieleza changamoto kubwa zinazowakabili wananchi, ikiwemo kupoteza mazao kutokana na uvamizi wa wanyama pori kama tembo na nyati wanaoingia katika makazi na mashamba, hali inayohatarisha shughuli za kiuchumi za kaya nyingi zinazotegemea kilimo.

Naibu Kamishna Joas Makwati alieleza kuwa  pamoja na suala zima la ujirani mwema kikao hicho  kitasaidia kuweka mikakati ya pamoja katika kutatua changamoto baina ya binadamu na wanyama pori wakali na waharibifu.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea na ziara za kukutana na wananchi katika vijiji mbalimbali ili kuimarisha ujirani mwema.m






 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO