RAIS MWINYI:SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA JUU.

RAIS MWINYI:SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA JUU. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali Ina Wajibu Mkubwa wa Kuendelea Kuwekeza katika Elimu ya juu ili kuzalisha Wataalamu wengi zaidi watakaochangia Maendeleo katika Sekta tofauti na Ustawi wa Wananchi. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan katika Kongamano la Kumuenzi Mkuu wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Tawi la Muhimbili (MUHAS) Rais wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Ndaki ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam. Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali inathamini Mafanikio Makubwa yaliofikiwa na Chuo cha Muhas tangu kuanzishwa kwake yanayochangia kuzalisha Wataalamu katika Sekta ya Elimu, Afya, Ufanyaji wa Tafiti na Utoaji wa...