RAIS MWINYI:SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA JUU.

 RAIS MWINYI:SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA JUU.


Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali Ina Wajibu Mkubwa wa Kuendelea Kuwekeza katika Elimu ya juu ili kuzalisha Wataalamu wengi zaidi watakaochangia Maendeleo katika Sekta tofauti na Ustawi wa Wananchi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipomuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu  Hassan katika  Kongamano la Kumuenzi Mkuu  wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Afya na  Sayansi Shirikishi Tawi la Muhimbili  (MUHAS) Rais wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Ndaki ya Chuo hicho  jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali inathamini Mafanikio Makubwa yaliofikiwa na Chuo cha Muhas  tangu kuanzishwa kwake  yanayochangia kuzalisha Wataalamu katika Sekta ya Elimu, Afya, Ufanyaji wa Tafiti na Utoaji wa  huduma za Afya kwa jamii.


Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amekipongeza Chuo cha Muhas kwa Mradi wa Upanuzi wa Miundonbinu ya Chuo hicho kupitia Mradi Unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa Ushirikiano na Benki ya Dunia na kuishukuru kwa Misaada yake kwa Tanzania.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi amekipongeza Chuo cha Muhas kwa Kuandaa Kongamano Maalum la Kumuenzi  Mkuu wa Kwanza wa Muhas Hayati Ali Hassan Mwinyi  na Uamuzi wa Kuanzisha Mfuko Maalum wa Ali Hassan Mwinyi Endowment Trust Fund ikiwa ni njia ya Kumuenzi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amekishauri Chuo cha Muhas Kuendeleza Mambo mazuri yalioanzishwa na  Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu ya Chuo hicho alichokiongoza kwa Miaka 17 .

Rais Dkt. Mwinyi amezindua Vazi rasmi lililokuwa likivaliwa na Mzee Mwinyi wakati akihudumu akiwa Mkuu wa Chuo pamoja na Kukabidhiwa Tuzo Maalum ya Kumuenzi kwa Utumishi wake Uliotukuka.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO