OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

Simiyu.

Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.

Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

"Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo vyake (TAWA na Jeshi la Polisi) na kuanza Oparesheni, lakini ilipofika tarehe 25/01/2025 oparesheni ya mkoa mzima ilifanyika Kwa ukubwa kuhakikisha inakabiliana na fisi wote waliokuwa wanasumbua wananchi" amesema Mhe. Kihongosi 

"Na Kwa taarifa njema ni kwamba tangu kuanza Kwa oparesheni hii vyombo vyetu vimeweza kudhibiti na kuua fisi 16 na ndio maana kwasasa mnaweza kuona hali imetulia" ameongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Simiyu.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima kuacha tabia ya kutembea  nyakati za usiku na alfajiri kwani ni nyakati ambazo wanyama fisi huwa katika mawindo yao.

Kwa upande wao wananchi wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima wameshukuru Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakisema kuwa hatua hiyo imeweza kuwarejeshea matumaini, utulivu na amani.

"Kwakweli tulikuwa tunasumbuliwa sana na haya mafisi ambayo yalikuwa yanauma watu, baada ya Serikali kusikia ikaweka ulinzi, kwakweli imetufanyia vizuri sana mpaka leo hatujawasikia tena tangu Askari waanze kuwashambulia hao fisi, mpaka leo hii tuna utulivu sana kwakweli tunashukuru sana"   amesema Mozo Mabula  mkazi wa Kijiji cha Mwamunhu kilichopo wilaya ya Itilima.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO