ZAIDI YA WATU 58 WANUFAIKA. NA USIMAMIZI WA MAJI TAKA MGODINI



📍Dodoma 

*Dkt. Mwanga Aongoza Kikao Ugeni Kutoka Sweden (SGU)*

Zaidi ya watu 58 wamenufaika na programu ya usimamizi wa maji taka migodini, inayotekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 chini ya usimamizi wa Taasisi ya Jiolojia ya Sweden (SGU) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA).

Hayo yamesemwa leo Oktoba 2, 2025 na Meneja wa Mradi wa Mafunzo ya Kimataifa kutoka SGU, Bi. Jonnina Karlsson, wakati wa ziara yake katika Ofisi za Wizara ya Madini na kushiriki kikao kilichoongozwa na Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Bi. Karlsson ameeleza kuwa hivi karibuni kutakuwa na fursa nyingine kupitia mradi wa PanGeo+ ambao utatoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Madini, hususan katika masuala ya kiufundi na usimamizi endelevu wa mazingira.


Aidha, Bi. Karlsson ameonesha nia ya kufahamu mahitaji ya wataalamu wa Sekta ya Madini nchini, ambapo imebainishwa kuwa miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na mwongozo wa ufungaji wa migodi kwa wachimbaji wadogo; Upimaji wa maji taka kabla ya kurejeshwa kwenye mazingira, hasa kwa wachimbaji wadogo na Matumizi ya teknolojia za _Remote Sensing_ na mifumo ya taarifa za jiolojia (GIS) katika utafutaji wa madini pamoja na kujenga uwezo wa watalaam katika mchakato wa kisayansi na kiuhandisi hususan katika kutathmin.

Mahitaji mengine ni kujengewa uwezo katika kupanga na kuonyesha kiasi cha ubora wa rasilimani kama vile madini yaani  _Resource modelling_ kwa ajili ya kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika utekelezaji wa miradi ya madini.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrhaman Mwanga ameishukuru SIDA kupitia SGU kwa kuwezesha mafunzo hayo ambayo yamelenga kuongeza uelewa kwa wataalamu wa madini kuhusu usimamizi wa madini pamoja na miundombinu ya maji taka migodini, hatua inayosaidia kulinda mazingira na kukuza uchimbaji endelevu.


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO