DKT. BITEKO ALITAKA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI KUONGEZA KASI YA UENDELEZAJI VITALU VYA MAFUTA NA GESI ASILIA*

📌 *Asema lengo ni kuendelea kuwa na uhakika wa usalama wa nishati nchini* 📌 *Azindua Mkakati wa Kwanza wa Muda mrefu wa Shirika (2025-2050)* 📌 *Asisitiza Jamii zinazozunguka miradi ya Mafuta na Gesi Asilia kutopuuzwa* 📌 *Apongeza Bodi na Menejimenti ya TPDC kwa kuipambanua Tanzania kama kitovu cha Mafuta na Gesi Asilia* 📌 *Balozi Sefue asema Mpango unakusudia kuongeza matumizi ya Gesi Asilia kutoka matumizi ya kawaida* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuongeza kasi ya uendelezaji wa Vitalu vya utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ikiwemo Mnazi Bay Kaskazini, Eyasi Wembere, Songo Songo Magharibi na Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) ili nchi iendelee kuwa na uhakika wa upatikanaji wa nishati kwa ajili ya soko la ndani na nje. Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Mkakati wa Muda Mrefu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wa miaka 25 (2024/25 hadi...