SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WOTE WANAOTUPA WATOTO.
SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WOTE WANAOTUPA WATOTO.
Dodoma
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaid Ali Khamisi (Mb) amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote ambao wamekuwa wakitupa watoto kwa lengo la kukwepa jukumu lao la msingi la kusimamia malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Mhe. Mwanaii ameyasema hayo Aprili 28, 2025 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Fakharia Shomar Khamis aliyetaka kujua kauli ya Serikali juu ya Wanawake wanaotupa watoto.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema Serikali inakemea na kulaani kitendo cha baadhi ya wanawake kutupa watoto kwa lengo la kukwepa jukumu lao la msingi la kusimamia malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
"Napenda jamii itambue kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wanawake watakaokutwa na hatia ya kutenda kosa hilo na wataadhibiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Sura ya 13, Kanuni ya adhabu Sura ya 16 pamoja na Sheria nyingine za Nchi zinazopinga suala hilo" ameeleza Naibu Waziri Mwanaidi
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi ametoa wito kwa jamii endapo itatokea mtu ameshindwa kutekeleza jukumu la malezi ya mtoto basi atoe taarifa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa hususani Ofisi za Ustawi wa Jamii ambao watawajibika kuweka mpango wa huduma mbadala kwa mtoto husika.
"Wanawake acheni tabia ya kutupa watoto na endapo itatokea kuna mtu ameshindwa kutekeleza jukumu la malezi ya mtoto basi atoe taarifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa husisani Ofisi za Ustawi wa Jamii ambao watawajibika kuweka mpango wa huduma mbadala kwa mtoto husika" amesema Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi.
Comments
Post a Comment