WANANCHI SAME WAASWA KUWAKUMBUKA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

WANANCHI SAME WAASWA KUWAKUMBUKA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Na Christina Thomas. 
Same, Kilimanjaro.

Wananchi wilayani Same wamesisitizwa kujenga utamaduni wa kuwakumbuka na kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu, (Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi) kwa kuwapatia msaada wa mahitaji ya msingi hususan chakula na mavazi ili nao wajisikie kuwa sehemu ya jamii na wenye thamani.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Kasilda Mgeni wakati alipotembelea na kutoa sadaka yake kidogo ya chakula na vinywaji kuelekea sikukuu ya Pasaka katika kituo cha Rafiki cha kulelea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi (Rafiki Children Centre) kilichopo wilayani humo.

"Hawa watoto hawakupenda kuwa katika mazingira haya, ila walijikuta wapo katika mazingira haya, Niwaombe sana wanasame, pamoja na raha zenu zote, mkumbuke kuwa watoto pia wamahitaji raha kama.unazozipata, basi zile raha unazozipata wape na watoto wa kituo hiki (Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi)". Alisema Mhe Kasilda Mgeni. 
Pia Mhe. Kasilda amewashukuru na kuwapongeza walezi na wasimamizi wa kituo hicho kwa kuonesha moyo wa upendo ambapo amewaahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika hali zote ili kufanikisha ndoto za watoto wanaolelewa kituoni hapo.

Naye Jeremia letus, ambaye ni Afisa ustawi wa jamii na Msimamizi wa kituo cha Rafiki amemshukuru mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Kasilda Mgeni kwa kuendelea kuwa sehemu ya faraja katika kituo hicho katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa wameweka kipaumbele kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo kuhakikisha wanapata elimu huku akiongezea kuwa wanakabiliwa na changamoto ya jengo kwa ajili ya watoto hao.

Kituo cha Rafiki cha kulelea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kina jumla ya watoto ishirini mpaka sasa.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO