WANANCHI KILIMANJARO WAISHUKURU SERIKALI KUPELEKA MADAKTARI BINGWA WA MACHO.
.png)
WALIOSUMBULIWA NA MACHO KILIMANJARO WAISHUKURU SERIKALI KUPELEKA MADAKTARI BINGWA WA MACHO. Na Mwandishi Wetu. Same, Kilimanjaro. Wananchi waliokuwa wakikabiliwa na matatizo ya kuona mkoani Kilimanjaro wameishukuru Serikali kwa kuwaletea madaktari bingwa wa macho kutoka nchini Marekani na kuwafanyia uchunguzi wa magonjwa hayo na ushauri wa kitaalam, tiba kwa upasuaji wa mtoto wa jicho na kuweza kuona upya. Madaktari hao ambao wamepiga kambi ya wiki mbili katika hospitali ya Wilaya ya Same ambapo watu zaidi ya elfu mbili (2000) wamefanyiwa uchunguzi huku wagonjwa zaidi ya tisini (90) wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho. Wakizungumza kwa nyakati tofauti hospitalini hapo mmoja kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho Bw. Idd Mlaki, Mkazi wa Kileo wilayani Mwanga alieleza kuwa kwa muda wa miezi sita alikuwa haoni tatizo ambalo lilianza ghafla ambapo kwa sasa mara baada ya kupata huduma hiyo hali yake ya kuona imerejea tena. “Macho yangu yalikufa ghafl...