JUHUDI ZA RAIS SAMIA, NEEMA KWA WANANCHI KUPITIA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE
JUHUDI ZA RAIS SAMIA, NEEMA KWA WANANCHI KUPITIA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE
Na Mwandishi Wetu.
Kilimanjaro.
Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni akiongozana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, leo machi 03, 2025 wametembelea mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, Ziara hii imelenga kukagua maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.



Mhe. Kasilda Mgeni amepongeza jitihada za serikali na wadau wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huu. Ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maji kama sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma za msingi kwa wananchi.
Mradi huu unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 9 Machi 2025. Uzinduzi huu utakuwa ni hatua muhimu katika juhudi za serikali kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watanzania, hususan katika maeneo ya Same, Mwanga na Korogwe.

Comments
Post a Comment