WAFANYABIASHARA WAONGEZE USAHIHI: RISITI KILA UNUNUZI

WAFANYABIASHARA WAONGEZE USAHIHI: RISITI KILA UNUNUZI Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX Na Musa Mathias Kipeo Online Media Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, amewataka wafanyabiashara kuendelea kutumia mashine za kielektroniki za kodi (EFD) na kuhakikisha kila mteja anapata risiti halali. Lengo kuu ni kupunguza mianya ya upotevu wa mapato ya serikali. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya, Kasilda alisisitiza kuwa ni jukumu la kila mfanyabiashara kutoa risiti kwa kila mauzo anayofanya, huku akiwaasa wateja kudai risiti wanaponunua bidhaa. “Tunatakiwa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara kutumia mashine za EFD, kutoa risiti kwa wateja huku wateja wakisisitizwa kudai risiti wanaponunua bidhaa, ili kulinda mapato ya serikali yasipotee,” alisema Kasilda. Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Same, Eliapenda Mwanri, alieleza kuwa taasisi hiyo imefanikiwa...