KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AIPONGEZA TARURA UJENZI KARAVATI BARABARA YA MPAKANI



Tunduma-Momba

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ally Ussi, ameipongeza TARURA kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa boksi karavati katika barabara ya Mpakani–Manga iliyopo Tunduma mkoani Songwe.

Ussi amesema hayo baada ya kukagua mradi huo na kuridhishwa na asilimia ya ujenzi iliyofikiwa, huku akibainisha kuwa miradi yote inayosimamiwa na TARURA ipo katika kiwango kizuri.

Kutokana na mahitaji makubwa ya vivuko kwa wananchi wa mji wa Tunduma, hususan Kata ya Chapwa na Mwakakati, serikali ilitenga fedha kutekeleza mradi huo.

Mwaka wa fedha 2023/24, Halmashauri kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, ilianza kutekeleza ujenzi wa boksi karavati mbili katika mitaa ya Mererani na Isanzo, barabara ya Mpakani hadi Manga.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi M/S Mante Company kwa gharama ya Shilingi 340,018,769.43 pamoja na ongezeko la Kodi ya Thamani ya Ongezeko (VAT inclusive).

Hadi sasa kazi zilizofanyika ni kuchimba msingi wa daraja, kusuka nondo, kumwaga zege na kujenga kuta za daraja, pamoja na kumalizia zege la juu la daraja (superstructure).


Meneja wa TARURA Wilaya ya Momba, Mhandisi Yusuph Shaban, amesema manufaa ya mradi huo ni kufungua mawasiliano kati ya Kata ya Chapwa na Mwakakati.

Ameongeza kuwa utarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa na biashara kwa kipindi chote cha msimu, kuongeza kipato kwa wakazi wa mji wa Tunduma na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa ujumla.


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO