NGORONGORO YAENDELEA KUVUTIA WAGENI WENGI MAONESHO YA MAGICAL 2025*



Na Hamis Dambaya ,Nairobi

Wageni kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kumiminika na kupata maelezo kuhusiana na vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji vilivyopo katika hifadhi ya Ngorongoro katika maonesho ya utalii ya Magical yanayoendelea jijini Nairobi nchini Kenya.

Maelezo kuhusiana na hifadhi ya Ngorongoro yamewavutia watembeleaji wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaotembelea maonesho hayo.

Upekee wa kreta ya Ngorongoro kutokana na uwepo wa wanyama mbalimbali ikiwemo "Big Five" wanaotambulika duniani pamoja na historia ya chimbuko la binadamu wa kale ni miongoni mwa mambo yaliyopendwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Afisa Masoko Mkuu Michael Makombe amesema kuwa ushiriki wa Ngorongoro katika maonesho hayo umeongeza wigo wa kujitangaza kimataifa na hivyo kuna matarajio makubwa ya kuongezeka kwa wageni wa kimataifa watakaotembelea hifadhi hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO