WATEJA 6,000 WAFUNGIWA UMEME NDANI YA SIKU 50 PWANI*



๐Ÿ“Œujio wa Magari mapya Pikipiki na bajaji vyaimarisha utoaji wa huduma kwa watejal

๐Ÿ“Œ*Kamati yaridhishwa na utendaji eneo la huduma kwa wateja mkoa wa Pwani*

Na. Salama Kasamalu

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepiga hatua katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wateja mkoani Pwani ambapo takribani wateja elfu 6 wamefikiwa na huduma ya umeme ndani ya siku 50.

Kuimarika huko kwa huduma kunatokana na ujio wa magari mapya, pikipiki na bajaji zilizotolewa Julai 2025 na Shirika hatua ambayo imeleta matokeo chanya. 

Akizungumza katika ofisi za TANESCO mkoa wa Pwani katika mwendelezo wa ziara za ukaguzi wa vituo vya huduma kwa wateja, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma kwa Wateja ya Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, Dkt. Lucy-Mary Mboma, amesema jitihada za TANESCO kuimarisha huduma kwa wateja zimeonesha matokeo chanya ikiwa ni pamoja na kufanikisha utatuzi wa changamoto za wateja ka haraka.

“Kupitia uwepo wa usafiri wa aina zote mliopewa na Shirika, tumeona ni namna gani wateja wanafikiwa haraka na changamoto zao zinatatuliwa ndani ya muda mfupi. Hii imerahisisha hata tathmini ya gharama za umeme, ambayo hapo awali ilichukua muda mrefu". Amesema Dkt. Mboma.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati hiyo Mhandisi Isack Chanji amesisitiza umuhimu wa kuendeleza miundombinu ya umeme ili kuhakikisha wateja wote wapya wanapata huduma haraka na viwanda vinaendelea kupata umeme bila tatizo.

Akimwakilisha Meneja Mkoa wa Pwani, Mhandisi Beatus Rwegoshora, amesema kuwa menejimenti ya Mkoa imepokea maelekezo ya kamati na ipo tayari kuyatekeleza.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kamati ya bodi ya huduma kwa wateja kukagua utendaji na utoaji wa huduma kwa wateja kwenye maeneo mbalimbali nchini




Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO