Posts

Showing posts from May, 2026

TARURA YAPATA DOLA MILIONI 65 KUTEKELEZA MIRADI YA DHARURA

Image
#Makandarasi wazawa wanufaika . Tabora Serikali imeiwezesha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupata dola milioni 65 kwa ajili ya utekelezaji wa matengenezo ya miundombinu ya barabara kupitia mfuko wa dharura (CERC). Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo katika mradi wa ujenzi wa daraja lenye urefu wa Mita 22 pamoja na barabara za maingilio zenye urefu wa Mita 290 kwenye  barabara ya Ndovelwa yenye urefu wa Km. 20.2 katika Manispaa ya Tabora. Mhandisi Seff amesema fedha hizo ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia uliotolewa kufuatia tathmini ya uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua za El-Nino za mwaka 2024. Amesema  tathmini hiyo ilibaini maeneo mengi ya barabara yaliyoharibiwa na hivyo kuhitaji matengenezo ya haraka ili kurejesha mawasiliano na huduma kwa wananchi. “Miradi hii inatekelezwa nchi nzima na kwa wastani utekelezaji wake umefikia asilimia 70. Kazi zote zina...

WAFANYAKAZI TARURA WAHIMIZWA KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA UFANISI LICHA YA MAFANIKIO

Image
‎Tabora ‎Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff, amewataka wafanyakazi wa Wakala huo kuendelea kuongeza juhudi, weledi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao licha ya pongezi wanazoendelea kupokea kutoka kwa wananchi kutokana na maboresho ya miundombinu nchini. ‎ ‎Mhandisi Seff ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TARURA uliofanyika mkoani Tabora, akisisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza bidii zaidi katika kuwahudumia wananchi. ‎ ‎"Tunapokea pongezi nyingi kutoka kwa wananchi kutokana na kazi nzuri inayofanywa na TARURA lakini mafanikio hayo yasitufanye turidhike. Tunapaswa kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuongeza juhudi ili kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi",  amesema Mhandisi Seff. ‎ ‎Ameongeza kuwa anatambua mchango mkubwa wa watumishi wa TARURA nchini kote, akibainisha kuwa jitihada zao zimekuwa na manufaa makubwa tangu k...

MTWARA YAFUNGUA FURSA MPYA KATIKA SEKTA YA CHUMVI

Image
- Serikali yapunguza gharama za leseni ya Madini Chumvi, wachimbaji wanufaika šŸ“Mtwara Mkoa wa Mtwara umeendelea kujidhihirisha kuwa kitovu muhimu cha uwekezaji katika sekta ya chumvi kutokana na uwepo wa fukwe zinazofaa kwa uzalishaji, maboresho ya mazingira ya biashara na ongezeko la uzalishaji linalofikia takribani tani 90 kwa majaruba manne katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji. Kutokana na hatua hiyo, wachimbaji na wazalishaji wa chumvi wameanza kunufaika na fursa mpya za kiuchumi kupitia kuongezeka kwa uzalishaji, ajira na upanuzi wa maeneo ya uzalishaji. Akizungumza katika mahojiano maalum, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Winnifrida Mrema, amesema sekta ya chumvi mkoani humo inaendelea kukua kwa kasi kutokana na kuimarika kwa shughuli za uzalishaji pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchakataji wa chumvi. Amesema maboresho hayo yanalenga kuongeza ubora wa chumvi kwa matumizi ya majumbani, viwandani na mifugo, huku yakichochea ajira kwa wananchi wa maeneo yana...

*RUVUMA YAPOKEA MAJIKO BANIFU 7,648 KWA BEI YA RUZUKU*

Image
šŸ“ *Songea , Ruvuma.* Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, leo Mei 25, 2026 amepokea rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited. Mradi huo unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia usambazaji wa majiko banifu yenye teknolojia ya kisasa kwa gharama nafuu kutokana na ruzuku inayotolewa na Serikali. Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa majiko banifu yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi pamoja na kulinda mazingira. Amesema matumizi ya majiko hayo yatasaidia kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa usio salama, ikiwemo moshi unaosababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji, hususan wanawake na watoto. Mheshimiwa Ahmed Ab...

*KARIBU NYUMBANI YABAMBA OLDUVAI

Image
.Washiriki zaidi ya 300 wameshiriki mbio fupi za kilomita 5 katika  bonde la Olduvai Ngorongoro kwa lengo la kutangaza vivutio vya asili vya Olduvai na Laetoli ambapo historia ya Binadamu wa Kale ilianzia. Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi kwenye tukio hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa Ngorongoro kwa kushirikiana na Cape to Cairo Marathon imefanya mbio hizo ili kuonesha utajiri wa utalii wa asili, historia, urithi wa utamaduni na  mambo kale uliopo Olduvai na Laetoli kama Nyumbani kwa asili ya Binadamu. Ameongeza kuwa Ngorongoro ni Nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kwa kuwa pumzi ya kwanza ya ndama kupigwa mhuri kabla ya kuhamia maeneo mengine safari yao huanzia Ndutu Ngorongoro. "Ngorongoro ni Nyumbani kwa asili ya binadamu kisayansi, Ni nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kila mwaka, ni nyumbani kwa Spinshi ya Ndege zaidi ya 500, ni nyumbani kwa Wanyama wakubwa watano, kiufupi eneo la Ngorongo...

*REA YAANDIKA HISTORIA LUDEWA*

Image
*šŸ“ŒYawasha umeme ukanda wa Nyasa kitongoji cha Nkanda* *šŸ“ŒYapongezwa kufikisha umeme kwenye mazingira magumu Njombe* *šŸ“ŒBodi ya REA yasisitiza wananchi kuchangamkia fursa uwepo wa nishati ya umeme* šŸ“Nkanda - Ludewa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijni (REA), unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa na watakaopewa zabuni ya kutekeleza miradi ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi. Hayo yamebainishwa leo Mei 25, 2026 na Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), wakati wa hafla ya kukagua miradi, kutembelea na kuwasha umeme kitongoji cha Nkanda kilichopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mradi uliokuwa unatekelezwa na Suma Jkt Electric Company Ltd.  Mha. Ahmed Chinemba amesema kuwa, mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji vya mwambao wilayani Ludewa unatekelezwa na mkandarasi M/S SUMAJKT ELECTRIC COMPANY LTD kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni ...

WANARUDI NYUMBANI CHIMBUKO LA ASILI YAO

Image
Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watalii wa ndani kutembelea hifadhi ya Ngorongoro hii ikimaanisha wanarudi nyumbani eneo ambalo ndilo pekee lenye ushahidi wa kisayansi usiotiliwa shaka kuwa ndio chanzo cha binadamu wa kale. Safari hii ni zamu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa  hilo Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam Rev, Dr. Elliona Kimaro aliyeongoza kundi la wanaume 300 kutoka mikoa mbalimbali nchini kutembea Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai (Urithi Geopark) na vituo vya hifadhi vilivyopo Ngorongoro  Akiwa na Ujumbe huo Dkt.  Kimaro amesema makundi mbalimbali kuhamasika kufanya utalii wa Ndani wanavutiwa na vitu mbalimbali ikiwemo kushuhudia uumbaji wa Mungu, kuona na kujifunza Chanzo cha asili ya Mwanadamu katika bonde la Olduvai na Laetoli, kuona Ikolojia ya hifadhi pamoja na utunzaji wa Mazingira kama vitabu vitakatifu vinavyohimiza. "Tumekuja Nyumbani Ngorongoro kwenye asili ya Mwanadamu tuki...

MADINI YABADILISHA MAISHA RUANGWA, WACHIMBAJI WATOKA ‘BUKU BUKU’ HADI MIRADI YA MAENDELEO

Image
šŸ“LINDI Wilaya  ya Ruangwa mkoani Lindi imeendelea kushuhudia mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kufuatia kuongezeka kwa shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Namungo unaomilikiwa na kampuni ya Elianje Limited, huku wachimbaji wadogo na wananchi wa maeneo yanayouzunguka mgodi huo wakinufaika kupitia ajira, biashara na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Ukuaji wa shughuli za uchimbaji katika mgodi huo umechangia kuboresha huduma za maji, elimu, afya na miundombinu, hali iliyobadili maisha ya wananchi ambao miaka michache iliyopita walikabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii. Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Lindi, Mhandisi Dickson Joram amesema hali ya wachimbaji na wananchi wa Namungo imebadilika kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na mwaka 2019 alipowasili katika eneo hilo. Amesema wakati huo shughuli za uchimbaji zilikuwa katika kiwango cha chini, huku wachimbaji wengi wakitumia njia duni za uzalishaji na kushindwa kumudu mahitaji m...

TANZANIA NA MAREKANI ZAENDELEZA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA SEKTA MUHIMU

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Andrew Lentz, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, huduma za kibalozi, biashara na uwekezaji, usalama, nishati pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya maendeleo. Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie S. Kanza, ambaye alishiriki katika majadiliano yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili. Aidha, pande zote mbili zilisisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya mazungumzo yenye tija kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.