WAZIRI KOMBO APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA KONSELI MKUU WA KENYA NCHINI




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Jamhuri ya Kenya nchini, Mhe. Mohamed Ramadhan Ruwange, katika kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kidiplomasia na kusisitiza dhamira yao ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kenya. Aidha, walikubaliana kuendeleza majadiliano ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika juhudi za kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Mhe. Kombo amempongeza Mheshimiwa Ruwange kwa uteuzi wake na amemuhakikishia ushirikiano wakati wote atakapokuwa anahudumu hapa nchini.

Naye Mhe. Balozi Ruwange ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano uliopo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, usafiri wa anga, miundombinu na utalii.

Maeneo mengine ni  kilimo, teknolojia ya habari na mawasiliano, ufugaji na uvuvi, elimu, nishati, ulinzi na usalama.


Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO