*KIKWETE: NIDHAMU NA UADILIFU NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA*


 DAR ES SALAM: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Riziwan Kikwete, amewataka viongozi wanaochipukia nchini kutumia elimu na mafunzo ya uongozi waliyoipata kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla.


Waziri Kikwete ametoa kauli hiyo leo Mei 15, 2026 aliposhiriki Mahafali ya Tisa ya Wahitimu wa Kozi za Uongozi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo pia aligawa vyeti kwa wahitimu wa programu mbalimbali za uongozi.

Kozi hizo zimehusisha mafunzo ya Wanawake Viongozi, Viongozi Wanaochipukia pamoja na kozi za uongozi katika madaraja tofauti kwa lengo la kukuza uwezo wa viongozi katika taasisi za umma na binafsi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kikwete amesema nidhamu na uadilifu ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa na kwamba viongozi wakizingatia maadili hayo wataweza kuleta mabadiliko chanya nchini na barani Afrika kwa ujumla.

“Nidhamu na uadilifu vikizingatiwa ipasavyo vitaweza kuiponya Tanzania na Afrika kwa ujumla,” amesema Waziri Kikwete.

Aidha, amesema kozi hizo zinazoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Vyuo vya Aalto cha Finland na Yale cha Marekani zina mchango mkubwa katika kuandaa kizazi cha viongozi wenye uwezo, weledi na maadili ya uongozi bora.

#KaziInaendelea





 

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO