Posts

Showing posts from January, 2026

MBEYA WAPOKEA BILIONI 42.6, KUPELEKA UMEME VITONGOJI 318*

Image
*📌Idadi ya vitongoji vyenye umeme Mbeya ni 1,970 sawa na asilimia 67%* *📌Mkandarasi atakiwa kutekeleza mradi huo kulingana Taratibu zilizowekwa* 📍Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kupeleka kiasi cha shilingi bilioni 42.6 mkoani Mbeya ili kupeleka umeme kwenye vitongoji 316 kupitia mradi wa HEP 2B unaotekelezwa mkoani humo ili wananchi wanufaike na nishati hiyo.  RC Malisa amesema mradi huo unakwenda kuleta tija na kuchochea maendeleo ya wananchi wa mkoa huo ambao wataunganishiwa umeme huo kuwawezesha kuendesha shughuli zao za kiuchumi.  "Gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000 tu. Nawaomba wananchi wa mkoa huu mtumie fursa hii ya kuunganisha umeme iliyoletwa na Serikali kupitia REA.," Amesema RC Malisa.  Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Bw. Frank Mugogo amesema jumla ya Vitongoji mkoa wa Mbeya ni 2,951 ambapo vitongoji vyenye umeme ni 1,970 sawa na asilimia 67%. ...

*AMBONI ADVENTURE RUN, FURSA YA KUTANGAZA MAPANGO YA AMBONI TANGA*

Image
Na Kassim Nyaki, Amboni Tanga. Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeshiriki na kudhamini mbio za AmbonI Adventure run zilizofanyika leo tarehe 31 Januari 2026 jijini Tanga kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii hususan mapango ya Amboni yanayosimamiwa na Mamlaka yah ifadhi ya Ngorongoro Mbio hizo za umbali wa kimomita 6, 10 na 20 ambazo zimehudhuriwa na wakimbiaji zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali nchini zimeanzia katika viwanja vya Shule ya Sekondari Galanos hadi Mapango ya amboni ambapo washiriki wa mbio hizo wamepata fursa ya kufanya utalii wa ndani katika mapango hayo. Kaimu meneja uhusiano wa Ngorongoro Hamis Dambaya ambaye ameshiriki mbio hizo kwa kukimbia kilomita 10 ameeleza kuwa  Ngorongoro imeamua kuungana na wadau mbalimbali kuendelea kutangaza vivutio vilivyoko katika mapango ya Amboni ili yaendelee kujulikana kitaifa na kimataifa na kuvutia wageni wengi kutembelea na kuona vivutio vinavyopatikana katika mapango hayo na kupataa taarifa mbalimbali ikiwemo histori...

NGORONGORO SAKO KWA BAKO NA TAASISI ZA ELIMU KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NA ELIMU YA UHIFADHI

Image
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro leo tarehe 30 Januari, 2026 imeendelea na kampeni ya kutoa elimu ya vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro na elimu ya uhifadhi endelevu kwa wanafunzi na walimu wa shule za Sekondari Manyara, Lowasa , Rift valley na Chuo cha Maendeleo ya wananchi FDC Mto wa Mbu ambapo taasisi zote zipo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

RC IRINGA ASISITIZA WANANCHI KUWALINDA WAKANDARASI NA VIFAA VYA UJENZI*

Image
*📌Mradi wa bilioni 32.3 kusambaza umeme kwenye vitongoji 214 vya mkoa wa Iringa* *📌Mkandarasi M/s Silo Power atakiwa kumaliza kazi kwa wakati* *📌Wateja 7,500 wataunganishiwa huduma ya umeme* *📌Asema umeme ni maendeleo, uchumi, huduma na biashara* 📍Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James, amewataka wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano kwa Wakandarasi wa miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ikiwemo kulinda miundombinu na vifaa vya ujenzi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na iweze kuleta tija na kuchochea maendeleo nchini.  RC James amebainisha hayo leo Januari 29, 2026 wakati Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikimtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya M/s Silo Power itakayotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye vitongoji 214 vya mkoa wa Iringa  ambapo mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu, kuanzia sasa. Vile vile, RC James amesema mkoa wa Iringa unamahitaji makubwa ya umeme kutokana na kuongezeka kwa viwanda ...

MHE. KHERI JAMES AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MKOA WA IRINGA

Image
Zaidi ya miti milioni 42 kupandwa katika maeneo mbalimbali  Ihemi - Iringa, Januari 29, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amezindua rasmi kampeni ya upandaji wa miti Mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha uhifadhi endelevu wa misitu. Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika katika eneo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Kijiji cha Ihemi kwa ushiriki wa viongozi wa serikali, wadau wa mazingira, taasisi mbalimbali pamoja na wananchi, ambapo zoezi la upandaji wa miti lilianza sambamba na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na misitu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Kheri James amesema kuwa lengo la uzinduzi ni kuendeleza utamaduni wa kupanda miti na  amesisitiza kuwa upandaji wa miti haupaswi kuishia kwenye kampeni pekee, bali uende sambamba na utunzaji wa miti hiyo ili kuhakikisha inakua na kuleta manufaa yaliyokusudiwa. “Miti inapandwa kwa malen...

DKT NCHIMBI AKAGUA UKARABARI WA JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo tarehe 29 Januari 2026, ametembelea na kukagua ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli, Posta Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais ambaye yupo Jijini Dar es Salaam kwa shughuli mbalimbali za kikazi amekagua maendeleo ya ukarabati pamoja na uwekaji wa vifaa na samani katika ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo. Baada ya ukaguzi huo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi, amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba ukarabati huo umekamilika kwa asilimia mia moja na Jengo litakuwa tayari kwa matumizi kuanzia tarehe 04 Februari 2026.

*KISHINDO CHA DKT. KIJAJI MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO.*

Image
Na Kassim Nyaki, Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 29 Januari, 2026 jijini Arusha amezindua bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na kuielekeza kusimamia uhifadhi, kubuni mazao mapya ya utalii na kuyatangaza na kuboresha huduma za maendeleo kwa wananchi wa  wilaya ya Ngorongoro. Dkt. Kijaji amebainisha kuwa hifadhi ya Ngorongoro ni eneo muhimu kiuhifadhi na moja ya maeneo yanayotambuliwa kama urithi wa dunia na UNESCO hivyo  ameiunda bodi hiyo kwa kuteua manguli wa kila sekta ili kufikia matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ya kuona uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii vinasimamiwa bila kuipoteza hifadhi hiyo. “Nimeteua wataalam kutoka sekta zote serikali na binafsi  ili muisaidie serikali katika kusimamia maeneo hayo kwani hifadhi ya Ngorongoro ina mvuto mkubwa duniani,hivyo ni jukumu lenu kutumia taaluma na weledi wenu katika kuhakikisha Ngorongoro inaendelea ...

EXCHANGE RATE VIWANGO ELEKEZI VYA KUBADILISHA FEDHA KIGENI LEO

Image

SIKU 100 ZA RAIS SAMIA: TARURA MKOA WA SHINYANGA YASAINI MIKATABA KUMI YA UJENZI WA BARABARA MKOANI HUMO

Image
. Dar es Salaam. Meneja wa TARURA Mkoa Shinyanga Mhandisi Avith Theodory amesema kuwa ndani siku 100 tangu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aingie madarakani katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Sita miradi 10 ya ujenzi wa barabara imesainiwa na tayari Wakandarasi wapo maeneo ya kazi 'site' wakiendelea na utekelezaji. Hayo ameyasema pembezoni mwa Mkutano wa Mwaka wa Barabara uliondaliwa na Chama cha Barabara Tanzania  (TARA) unaondelea kufanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam. Amesema mikataba hiyo ya ujenzi pamoja na mambo mengine inahusu kurudisha mawasiliano yaliyokatika hasa maeneo ya vijijini kutokana na athari za mvua kubwa zilizonyesha mwaka 2025/26. Kwa mujibu wa Mhandisi Theodory mikataba hiyo pia inahusu ujenzi wa makalavati pamoja na madaraja makubwa mawili na kuongeza kuwa miradi hiyo ina faida kubwa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi hususani wakulima na wafugaji mkoa...

TANZANIA YAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA JUKWAA LA WIKI YA NISHATI INDIA

Image
Na Mwandishi Wetu Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ameshiriki katika mdahalo wa Mawaziri kuhusu uwekezaji na uimarishaji wa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya mafuta na gesi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nishati ya India (India Energy Week – IEW 2026) yanayoendelea kufanyika Goa, India. Akizungumza katika mdahalo huo uliofanyika leo Januari 28, 2026, Mhe. Makamba ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kuzingatia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi. Amebainisha kuwa tafiti za kuchukua taarifa za mitetemo zinaendelea kufanyika katika vitalu vya Eyasi–Wembere, Lindi na Mtwara, sambamba na kukamilisha majadiliano na wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo Mradi wa Gesi Asilia Kimiminika (LNG). Aidha, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika miradi ya usambazaji wa gesi kwa matumizi ya viwandani, uzalishaji wa umeme, matumizi ya majumbani pamoja na kuendesha magari. ...

WIZARA YA MAJI YAFUNGUA MILANGO KWA SEKTA BINAFSI KULETA MAGEUSZI SEKTA YA MAJI.

Image
Na Deborah Lemmubi -Dodoma. Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema kuwa Wizara hiyo imefungua milango kwa wadau mbalimbali wa Sekta binafsi ili kushirikiana na Wizara katika huduma ya utoaji Maji na kufanya mageuzi kwa kuhakikisha vijiji 1575 ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji vinafikiwa na huduma hiyo na kuondokana na changamoto ya maji inayopatikana kwa baadhi ya vijiji. Waziri Aweso ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Januari 28,2026 wakati akielezea mafanikio mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Wizara hiyo katika suku 100 za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.  Pamoja na kusema ufungaji wa mita za malipo ya kabla nayo pia itachangia kupunguza changamoto zilizopo katika huduma maji ikiwemo ubambikiaji wa ankara na upotevu wa maji utatatuliwa kwa kutumia Teknolojia. "Tumebadilisha Sera kwa maelekezo ya Mhe Rasi ambayo sasahivi Sera ya Wizara ya maji imeweza kuwakaribisha Sekta binafsi kuja kushirikiana pamoja nasi ili kufanya mageuzi katika Wizara ya maji". Aidha Waziri Aweso ames...

REA WAMTAMBULISHA MKANDARASI ATAKAEFIKISHA UMEME VITONGOJI 175 MTWARA

Image
Katika kutekeleza kauli mbiu ya “Vitongojini kama Mjini”, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kumtambulisha mkandarasi wa atakaesambaza umeme kwenye vitongoji 175 mkoa wa Mtwara. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amewataka REA kumsimamia vema mkandarasi ili aweze kukamilisha kwa wakati huku akiwahakikishia ushirikiano. “Nahitaji Ofisi ya Mkoa ipatiwe mpango kazi wa mkandarasi ili tuweze kufuatilia mwenendo wa utekezwaji wa mradi. Kwa ile miradi iliyokamilika, REA toeni taarifa ili izinduliwe wananchi waweze kuanza kuitumia. Umeme ni uchumi, unachochea ajira na uwekezaji.” Alieleza Kanali Sawala Meneja Usimamizi  wa miradi REA, Mha. Deogratius Nagu ameeleza kuwa mradi huo wa kusambaza umeme kwa ngazi ya vitongoji kwa Mkoa wa Mtwara itatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2026 mpaka Januari 2029 ukitarajiwa kunufaisha wananchi 5,646 Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Dieynem inayotekeleza mradi huo, Mha. Novatus Lyimo ame...

TARURA YASHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA BARABARA

Image
Dar es Salaam Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imeshiriki mkutano wa mwaka wa barabara uliondaliwa na Chama cha Barabara Tanzania (TARA). Mkutano huo wa siku nne uliofunguliwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega umefanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi.  Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Ulega amesema kuwa maboresho ya Sekta ya usafirishaji Tanzania inabaki kuwa ni kipaumbele cha Serikali na ni maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.  "Serikali inaendelea kuwekeza katika upanuzi, maboresho na matengenezo katika mtandao wa barabara za Mijini na Vijijini kwa kutoa fedha katika matengenezo hayo, kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi, ustahamilivu wa mabadiliko ya tabianchi, uendelevu wa mazingira katika maendeleo ya Miundombinu nchini." amebainisha Mhe. Ulega Akiongea na Waandishi wa Habari pembezoni mwa mkutano huo Mhandisi Mshauri Pharles Ngelej...

*TANESCO YAFANYA UKAGUZI WA MITA KITAALAMU KUBAINI UKWELI MALALAMIKO YA UMEME KUISHA HARAKA YAGUNDUA MITA ZIPO SAWA*

Image
📌 Ni kufuatia malalamiko ya baadhi ya wateja kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari 📌 Chanzo cha tatizo kwa mita zilizokaguliwa chatajwa kuwa ni uchakavu wa wiring za ndani ya nyumba na tabia holela za matumizi ya umeme 📌 Shirika kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wananchi. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanya ukaguzi wa kitaalamu wa mita za umeme kwa baadhi ya wateja waliowasilisha malalamiko hayo kwa njia za mitandao katika maeneo ya Tabata Kimanga na Kimara Suka jijini Dar es Salaam. Malalamiko hayo yaliibuliwa na baadhi ya wananchi mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu madai ya umeme kuisha haraka bila sababu ya msingi. Zoezi hilo lilifanyika Januari 27, 2026, likiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, akiambatana na timu ya wataalamu wa Shirika, kwa lengo la kubaini chanzo halisi cha changamoto hiyo na kujiridhisha kuhusu ufanisi wa utendaji wa mita za wateja. *Matokeo ...

MAONI YA WADAU YAKUSANYWA UABZISHWAJI BODI YA WAJIOSAYANSI*

Image
*Rasimu ya Waraka wa Mapendekezo ya Baraza la Mawaziri ipo Tayari : Dkt. Kiruswa* Na Wizara ya Madini, Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Madini inaendelea na mchakato wa kuanzisha Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Jiosayansi Tanzania (Tanzania Geoscientists Registration Board – TGRB), ambapo kwa sasa ipo katika hatua ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau kabla ya kuanzishwa rasmi kwa bodi hiyo. Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema hayo leo Januari 28, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukene, Mhe. Stephano Luhende, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha mchakato wa kuanzisha bodi hiyo ili kuongeza ufanisi katika sekta ya madini nchini. Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa baadhi ya taratibu tayari zimekwisha tekelezwa, ikiwemo uandaaji wa rasimu ya Waraka wa Mapendekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu kuanzishwa kwa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Jiosayansi Tanzania. Amefafanua kuwa kwa sasa Wizara ya Madini inaendelea na zoezi la kukusanya...