Posts

Showing posts from 2026

WATUMISHI REA WASHIRIKI SITE TRUST MARATHON NAMTUMBO 2026

Image
πŸ“Œ*Watumia fursa hiyo kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia* πŸ“ Namtumbo, Ruvuma Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo tarehe 24 Oktoba, 2026 wameshiriki mbio za Site Trust Marathon zilizofanyika wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Wakala zinazolenga kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. Marathon hiyo imeandaliwa na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Juma Homera, kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii katika shughuli za michezo na maendeleo. Ushiriki wa REA katika marathon hiyo ni sehemu ya mkakati wa Wakala wa kuwafikia wananchi kupitia majukwaa mbalimbali ili kuongeza uelewa na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za nishati safi ya kupikia nchini. Mwisho

ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU

Image
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewataka watumishi wake waliohudhuria mafunzo ya kiutumishi kwa siku tano mjini Dodoma kuyafanyia kazi mafunzo yao ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji. Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia huduma za shirika Aidan Makalla ametoa rai hiyo kwa watumishi has wakati akifunga mafunzo ya wiki moja yenye lengo la kuwajengea watumishi uelewa kuhusu utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uhifadhi, Utoaji wa huduma bora kwa wateja na nidhamu mahala pa kazi Makalla amesema mamlaka imewekeza mtaji kwa watumishi hao kwa kuwapa elimu hiyo ya utumishi, maadili, uwekezaji,afya ya akili na itifaki ikiamini kwamba mafunzo ndiyo nyenzo muhimu katika uwajibikaji. “Sisi viongozi wa mamlaka ni kama wazazi tuna wajibu wa kuwapa mafunzo ili msiharibikiwe na baadaye mamlaka ikaja kulaumiwa, yatumieni mafunzo haya kuyajenga katika kazi zenu,”alisema Makalla. Hii ni awamu ya Pili kwa mwaka huu wa fedha kwa Mamlaka ya...

TANZANIA NA ANGOLA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA

Image
Tanzania na Angola zimeazimia kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kubaini fursa mpya za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili. Dhamira hiyo imejidhihirisha katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. TΓ©te AntΓ³nio. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, pamoja na kubaini fursa mpya katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa pande zote. Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya Tanzania na Angola ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za maendeleo na kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

TANESCO KUIWEZESHA KAMPUNI YA HWTZ MEGAWATI 200 KUTEKELEZA MRADI WA UZALISHAJI UMEME

Image
πŸ“ŒWaziri Homera afanya Ziara katika Kongani ya Viwanda Mkoani Ruvuma chini ya muwekezaji HWTZ kutoka China πŸ“ŒAtoa rai kwa TANESCO kuharakisha mazungumzo na muwekezaji ili kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo πŸ“ŒMradi wa kamapuni HWTZ ukikamilika kuzalisha zaidi ya Megawati 2,000 Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Juma Homera amesema Shirika la umeme Tanzania TANESCO linatarajia kuingia makubaliano na muwekezaji kutoka  Kampuni ya Hongwang Tanzania Holdings (HWTZ ) kutoka China  kumpatia  jumla ya Megawati 200, kwa ajili ya ujenzi wa Mradi mkubwa wa kuzalisha zaidi ya megawati 2,000 za umeme kwa kutumia makaa ya Mawe na nishati ya jua Mkoani Ruvuma. Akizungumza Oktoba 23, 2026 wakati wa ziara yake katika kongani ya viwanda inayojihusisha na uwekezaji wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji Umeme, Kiwanda cha  Alminium pamoja na  Chuma , Waziri Homera ametoa rai kwa TANESCO kuharakisha mchakato wa kuingia makubaliano ili mradi huo uanze kutekelezwa kwa haraka kw...

TARURA KAKONKO YAKABIDHI MIKATABA 23 KWA VIKUNDI VYA KIJAMII KUFANYA MATENGENEZO YA KAWAIDA YA BARABARA

Image
Kankonko, Kigoma Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Kakonko imekabidhi Mikataba (23) kwa vikundi vya kijamii kwa lengo la kufanya matengenezo ya kawaida ya barabara yenye thamani ya shilingi milioni 211 kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Akikabidhi mikataba hiyo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Zuma Ally amevitaka vikundi hivyo kufanya kazi kwa bidii kwani ni vikundi vya mfano na hivyo wananchi wengine waweze kunufaika na shughuli hizo za CBRM. Amesema awali fedha hizo zilikuwa zikilipwa kwa wakandarasi wakubwa kutoka nje ya wilaya hivyo watumie fursa hiyo kufanya kazi na kujiimarisha kiuchumi. Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kakonko Bw. Ndaki Mhuli amevitaka vikundi hivyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maelekezo yote watakayopewa na wataalam wakati wanatekeleza kazi hizo. “Wana vikundi mnatakiwa kuhakikisha barabara zinakuwa safi na zinapitika wakati wote, pia mnatakiwa kuomba kazi mbalimbali zinazotangazwa na halmashauri ili kuboresha ...

MHE. SALOME AKUTANA NA KAMPUNI ZA CHINA KUJADILI UWEKEZAJI KATIKA MAFUTA, GESI ASILIA NA NISHATI JADIDIFU*

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome  Makamba, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kampuni mbili kutoka China kwa lengo la kujadili  uwekezaji katika sekta ya nishati nchini, hususan katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya gesi pamoja na miradi ya nishati jadidifu. Katika kikao kilichofanyika Oktoba 23, 2026, katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, Dar es Salaam, Mhe. Salome amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ChuanQing Drilling Company, Bw. Liu Chang Xu, yaliyolenga kujadili fursa za uwekezaji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia, ujenzi wa miundombinu katika mkondo wa chini wa sekta ya petroli pamoja na miradi ya nishati jadidifu, hususan nishati ya jua na jotoardhi. Pia, Mhe. Salome amezungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kwala Industries, Bw. Janson Huang, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Kinyerezi, Dar es Salaam, hadi Ch...

WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ROBO YA KWANZA 2026/27

Image
Dodoma, Oktoba 22, 2026 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, leo Oktoba 22, 2026, amewasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Nishati kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27, katika sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia. Kikao hicho kimefanyika katika Kumbi za Bunge jijini Dodoma, chini ya uenyekiti wa Mhe. Subira Mgalu, ambapo Wizara imewasilisha maendeleo ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazohusu utafiti, uzalishaji na matumizi ya mafuta na gesi asilia nchini. Katika maeneo ya vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2026/27, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeeleza hatua za utekelezaji wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (Tanzania Liquefied Natural Gas – TLNG), kuimarisha utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za petroli katika vitalu vya kimkakati vya Lindi- Mtwara, Songo Songo Magharibi, Eyasi- Wembere na Mnazi Bay Kaskazini. Aidha, TPDC imeeleza utekelezaji ...

KAPALATA AISHAURI SERIKALI KUREJEA MUUNDO WA WIZARA YA MADINI NA SHERIA YA MADINI ILI KUAKISI NA KUTAFSIRI SEKTA YA MADINI KUENDANA NA MSTAKABALI WA DIRA YA MAENDELEO TAIFA HADI 2050

Image
πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Asema kwa kuwa sekta ya madini inakua kila kukicha na inatafrisiwa kwa kauli mbiu kuwa madini ni maisha na utajiri kama ilivyo sekta ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, ni muhimu sana bila kuchelewa kurejea muundo wa wizara ya madini na sheria ya madini ili kuakisi na kutafsiri sekta ya madini kuendana na mstakabali wa dira ya maendeleo ya taifa hadi 2050 na maono ya wizara ya madini hadi 2030 kama mojawapo ya sekta za kimkakati za maendeleo ya taifa ili kuleta tija kwenye tasnia ya madini na kuitafsiri tasnia hii kibiashara pia na sio kirasilimali kama ilivyo sasa kwa kuongeza nguzo (pillars) mpya za maendeleo ya madini ili pamoja na mengineyo nguzo zilipo na nguzo mpya ziwe imara na thabiti kwa kulenga kila aina ya madini yanayopatikana nchini.  πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Aeleza kuwa tume ya madini iliyopo sasa pamoja na mengineyo iwe na idara kubwa mbili, yaani idara ya rasilimali madini (mineral resource and reserves department) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kutafuta, kuratibu, kulinda, ku...

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA UWEZO WA KUKABILIANA NA MAAFA*

Image
Na Mwandishu Wetu Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuimarisha uwezo wa nchi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa kutoa mafunzo kwa Timu ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura, inayolenga kuongeza ufanisi wa uratibu na utekelezaji wa hatua za kukabiliana na matukio ya dharura. Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Oktoba, 2026, jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maudhui ya Ndani, Bw. Condrad Millinga, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu wakati akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Jim James Yonazi. Bw. Milinga amesema, mafunzo kwa timu hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha mfumo wa usimamizi wa maafa nchini, hususan katika kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa, taarifa sahihi zinapatikana na tathmini za madhara zinafanyika kwa wakati ili kuokoa maisha, kulinda mali na kupunguza athari kwa jamii. “Timu hii ina majukumu mbalimbali, yakiwemo kushiriki katika operesheni za kuk...

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU NA UPATIKANAJI WA MAFUNZO TARAJALI

Image
Serikali inaendelea kuweka mkazo maalum kwenye kuboresha mfumo wa uratibu na upatikanaji wa mafunzo ya utarajali (internship) kwa kuwapatia wahitimu wa kada mbalimbali, uzoefu na ujuzi unaohitajika kwa lengo la kuwafanya wahitimu hao kuwa shindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam Oktoba 22, 2026, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, amesema maboresho yanayoendelea kufanyika ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyoyatoa wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma (C-COEs Forum 2026) tarehe 28 Septemba, 2026 jijini Arusha. Katika kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya...

DKT. HOMERA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI

Image
πŸ“Œ*Wajadiliana maeneo ya ushirikiano katika sekta ya nishati* Dar es Salaam, Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, kuhusu maeneo mbalimbali ya ushirikiano na uwekezaji katika sekta ya nishati, hususan umeme, nishati jadidifu, mafuta na gesi asilia pamoja na nishati safi ya kupikia. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo, Oktoba 22, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam, Dkt. Homera amesema Tanzania inahitaji wawekezaji katika utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kujazia gesi asilia iliyoshindiliwa kwenye vyombo vya usafiri (CNG). Aidha, amesema Tanzania inahitaji ushirikiano wa kitaalamu na kiteknolojia katika ujenzi, uendeshaji na usimamizi wa viwanda vya kusafisha mafuta  hususan wakati huu ambapo nchi ipo katika mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kusafisha mafuta mkoani Tanga. "Katika shughuli za utafut...

TANZANIA YANG'ARA AFRIKA UTASHI WA UONGOZI KATIKA UWEKEZAJI SEKTA YA YA MAJI

Image
Tanzania imeng'ara katika umoja wa Mataifa Afrika kwa utashi wa Uongozi katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia serikali yake imetoa kipaumbele kwa sekta ya Maji na kutanga fedha za kutekeleza miradi pamoja na usimamizi thabiti katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya uhakika ya maji safi na salama na kupiga hatua za haraka maeneo ambayo yalikua na changamoto kubwa kufikiwa na maji wakati kazi ya kuendelea kusambaza maeneo yote ikiendelea kwa kasi. Rai hiyo imetolewa na viongozi wa Afrika katika mkutano wa Maraisi, Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Maji jijini Luanda nchini Angola kwenye Mkutano wa Maji kama Kiungo cha Amani Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki mkutano Mkutano huu leo tarehe 22 Oktoba 2026 unaongozwa na Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimwakilisha...