Posts

Showing posts from March, 2026

TARURA YATEKELEZA UJENZI WA KM 56 ZA BARABARA ZA LAMI ILALA KUPITIA DMDP II

Image
‎Dar es Salaam  ‎ ‎Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara zaidi ya Kilomita 56 kwa kiwango cha lami na zege kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mkoani humo. ‎ ‎Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Ilala, Mhandisi Grayson Nzunda amesema kuwa miradi inayojengwa ni barabara za lami na zege,  mifereji ya maji ya mvua, makalavati, njia za waenda kwa miguu, uwekaji wa taa za barabarani pamoja na kuweka alama za barabarani ambapo mradi unagharimu shilingi Bilioni 138. ‎ ‎“Hapa tulipo ni maeneo ya Kivule tupo  kukagua ujenzi wa barabara zenye urefu wa Kilomita 12, barabara ya Kivule-Majohe Junction Km 2.79 inajengwa kwa kiwango cha zege na barabara ya Kitunda-Kivule-Msongola Km 9.95 inajengwa kwa kiwango cha lami, mradi umegharimu shilingi Bilioni 30 kati ya Bilioni 138 za wilaya nzima ya Ilala", ...

*FUKUO LA KUFUKUA MAAJABU YA NGORONGORO LAFUKULIWA*

Image
Waswahili husema "Dunia ni jumba la maajabu  " Ngorongoro haiishiwi maajabu , Ni kama vile lile fukuo la kufukulia maajabu ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro limefukuliwa, hii inatokana na enzi mpya za msimu kwa waongoza utalii (Tour Guide) nane kushiriki kwenye fainali za _Safari Field Challenge_ kwa mwaka 2026 zitakazofanyika Ngorongoro  Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro inadhamini mashindano hayo ambapo waongoza utalii wanaoshiriki shindano walipatikana kwa kufanyiwa mchujo na kupatikana washindi nane (08) ambao katika shindano hilo watapita kwenye vivutio ambavyo ni maajabu ya kustaajabisha na kutambua uwezo wao katika umahiri wa maarifa, ubinifu, ustahamilifu,  akili na uwezo wao wa kukabiliana na vikwazo katika safari za kitalii mbugani. Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Kamishna Msaidizi mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameleza kiwa shindano hilo litatumika kuionesha dunia kuwa...

MTI MMOJA, ENEO AMBALO SIMBA HULITUMIA KWA HONEYMOON KRETA YA NGORONGORO.*

Image
Unaweza kustaajabu lakini ukweli upo hivyo, ukitaka kuwaona simba wakiwa katika harakati za kuongeza familia fika katika  Kasoko ya Ngorongoro eneo la mti mmoja ambalo limezungukwa na vichaka, miti na nyasi za wastani. Eneo hili ni maarufu sana kwa waongoza utalii kutokana na makundi ya simba waliopo katika hifadhi hiyo kupenda kupumzika  na hasa wanapokuwa katika msimu wao wa kujamiina ama kutafuta watoto na kuongeza familia. Simba hupenda kujamiiana mara baada ya kushiba ambapo zoezi hilo linafanyika mda wowote mchana au usiku. Tofauti na Binadamu ambapo Kazi Ngumu hufanywa na wanaume, kwa Simba ni tofauti, kazi ya kutafuta chakula ama Mawindo kwa ajili ya msosi wa familia huongozwa na simba jike ambapo mara baada ya kuhisi njaa na tamaa ya kujamiina huamua kutafuta chakula ili kwanza kushiba halafu kuingia kwenye harakati ya kuongeza familia. Wakati wa mawindo simba huchagua chakula cha kushiba na hapa ina maana simba hahangaiki sana na wanyama wadogo wadogo kama swala kwan...

*NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA TANESCO MKOA WA SHINYANGA*

Image
📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia nishati safi umeme kupikia Na Mwandishi Wetu, Kahama Naibu Waziri wa Nishati Mh. Salome Makamba amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kutatua changamoto zao kwa haraka. Akizungumza leo tarehe 27, Machi 2026 wakati wa hafla ya kukakabidhi vitendea kazi hivyo iliyofanyika katika Manispaa ya Kahama Mkaoni Shinyaga Mhe. Salome amesema  hatua hiyo ya kukabidhi vitendea kazi hivyo ni kuyaishi maono ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Umeme wa uhakika. Amesema vitendea kazi  hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na kuwawezesha kutatua changamoto za wateja kwa wakati.  “Kupitia vyombo hivi vya usafiri vitakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika kumfikia mteja kwa haraka na kumhudumia, ni...

TANZANIA NA ISRAEL ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA ZA KILIMO NA AFYA

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema Israel imekuwa mshirika muhimu katika sekta mbalimbali nchini, ikiwemo kilimo, afya, ulinzi na usalama, hali inayochangia kuimarika kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesema hayo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, wakati akipokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Israel nchini, Mheshimiwa Gideon Behar, mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya. Mhe. Kombo amempongeza Balozi Behar kwa uteuzi wake na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini katika kipindi chote cha utumishi wake nchini. Aidha, ameipongeza programu ya MASHAV ya Israel inayotoa mafunzo ya vitendo kwa vijana wa Kitanzania kwenye mashamba nchini humo, na kupendekeza wataalamu wa Israel kuja kufundisha moja kwa moja katika vyuo vya kilimo nchini, ikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Amebainisha ...

WAKALA WA VIPIMO WADHAMIRIA KUTOKOMEZA LUMBESA*

Image
*Na WMA – DODOMA* Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuanza ukaguzi wa mazao ya shamba na kupambana zaidi na ufungashaji wa mazao hayo kwa mtindo wa lumbesa. Akifungua Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa WMA, Machi 27, 2026 jijini Dodoma, Kihulla amewasisitiza wajumbe wa Baraza hilo kufikisha ujumbe huo kwa watumishi wote katika maeneo yao kuanza kutekeleza jukumu hilo kikamilifu. “Lakini tunapotekeleza majukumu haya, tuhakikishe haki katika biashara na kulinda mapato ya Serikali,”ametahadharisha. Amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026, WMA imepata mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kumlinda mlaji kupitia uhakiki wa vipimo lakini pia kumekuwepo na changamoto kadhaa. Akidadavua, amesema mafanikio yaliyopatikana yametokana na juhudi, weledi na ushirikiano wa watumishi wote wa Wakala hivyo amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya. “Pamoja na mafanikio hayo, bado...

TANZANIA NA SHIRIKA LA IFC KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA BINAFSI NA UWEKEZAJI

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) zimethibitisha azma ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza sekta binafsi, uwekezaji na uchumi endelevu kwa manufaa ya pande zote mbili. Hayo yameelezwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki, Mary Porter Peschka, yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kombo amepongeza mchango mkubwa wa IFC katika kuimarisha sekta ya fedha nchini, hususan kupitia usaidizi kwa benki za NMB, CRDB na NBC. Amesema ushirikiano huo umeongeza upatikanaji wa mikopo na mitaji, na kuwa msaada muhimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Aidha, Serikali imetambua mchango wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) katika maendeleo ya miundombinu, ikiwemo huduma za ushauri kwa miradi ya kimkakati kama mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar...

MRADI WA DMDP II KUJENGA KILOMITA 42.78 ZA LAMI KIGAMBONI

Image
Dar es Salaam  Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara Kilomita 42.78 kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika kata za Mjimwema, Kibada, Kigamboni, Vijibweni na Somangila zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Edgar Tumsifu ambapo amesema kuwa mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni 110 utekelezaji wake umefikia asilimia 30 huku tayari umeshaanza kuleta matokeo kwani barabara zilizokuwa na changamoto zimeshaanza kufanyiwa kazi na zikikamilika wananchi watanufaika na miundombinu hiyo. "Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu, TARURA Kigamboni tuna mtandao wa barabara Km 1035 kati ya hizo barabara za lami ni Km 10 lakini kupitia DMDP II imetuletea Km 42.78 kwahiyo tutakuwa na zaidi ya Km 50 za barabara za lami mpaka kufikia ...

FANYENI KAZI KWA BIDII, UPENDO NA USHIRIKIANO KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI - PROF. SHEMDOE

Image
Na OWM – TAMISEMI, Dodoma  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM– TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa OWM- TAMISEMI kufanya kazi kwa bidii, upendo, ushirikiano, pamoja na ubunifu katika utendaji wao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Prof. Shemdoe ametoa wito huo jana Machi 26, 2026 wakati  akifungua  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa OWM– TAMISEMI uliofanyika  Jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi. “Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku,” amesema Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiw...

TANZANIA YAPONGEZWA KATIKA JUHUDI ZA MABADILIKO YA NISHATI MKUTANO WA ZIMEC 2026*

Image
*Kitwe , Zambia* Rais wa Jamhuri ya Zambia Dkt. Haikande Hichilema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kutekeleza Ajenda ya Mabadiliko ya Nishati ( Energy transition)  Barani Afrika. Rais, Dkt. Hichilema alitoa pongezi hizo Machi 26, 2026 wakati anafunga mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati (ZIMEC) uliofanyika kwa siku mbili nchini Zambia. Dkt. Hichilema alisema kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, mkakati uliopata msukumo mkubwa kutoka kwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan. Rais , Dkt.Hichilema aliongeza kuwa katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika Tanzania inatekeleza ushirikiano wa kimkakati na Zambia kwa vitendo kupitia  sera rafiki na miradi ya miundombinu inayounganisha kanda nzima. Dkt. Hichilema alipongeza kuhusu  mpango wa wizara ya migodi na maendeleo ya madini nchini Zambia kwa kuweka lengo la uzalishaji wa tani milio...

BALOZI MTEULE MAULIDAH HASSAN AAGWA NA WAZIRI KOMBO, AAHIDI KUIMARISHA DIPLOMASIA YA TANZANIA NA OMAN

Image
Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Maulidah Hassan, amefanya ziara ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo amempongeza Balozi Maulidah kwa kuaminiwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mchango wake alioutoa alipokuwa Msaidizi Binafsi wa Rais katika masuala ya diplomasia.  Aidha, amemsisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji na utalii, pamoja na kulinda maslahi ya Watanzania wanaoishi nchini humo, huku akimhimiza kutumia uzoefu wake kuendeleza uhusiano huo. Kwa upande wake, Balozi Maulidah amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani aliyompa na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu. Amesema pia kuwa amedhamiria kuendeleza diplomasia ya uchumi na kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzani...

*KAMATI YA BUNGE YAPITISHA RANDAMA YA MADINI MWAKA 2026/27*

Image
✅️ Madini Yachangia Asilimia 57 ya Mauzo Yote ya Bidhaa Zisizo za Asili Nje ya Nchi ✅️ Makusanyo mpaka Februari 2026 Yafikia Shilingi Bilioni 880 ✅️ GST Yakidhi Vigezo Kuendelea Kuwa na Ithibati Mpaka 2029 ✅️ Waziri Mavunde Asisitiza Ununuzi wa Helikopta ya Utafiti, Mipango Iko Pale Pale 📍 Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Machi 26, 2026 imepitisha Randama ya Wizara ya Madini kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma, ambacho pia kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Wizara kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026 kwa mwaka 2025/26. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Wizara kwa namna inavyosimamia utekelezaji wa majukumu yake yaliyopelekea kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa kufikia asilimia 12.7 katika robo ya tatu ya Julai hadi Septemba 2025, ikiwemo kuibua miradi mipya na shughuli za utafiti,...

MHANDISI MATIVILA AKAGUA MIRADI YA DMDP II, ATOA WITO UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU

Image
📌TARURA kujenga takribani Km. 250 za barabara Manispaa zote za Dar es Salaam ‎ ‎Dar es Salaam ‎ ‎Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amesema Serikali kupitia TARURA inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu mkoa wa Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wake ili idumu kwa muda mrefu. ‎ ‎Ameyasema hayo ‎wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa DMDP II katika Manispaa za Ubungo na Kinondoni, akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ili kuboresha miundombinu na maisha ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. ‎ ‎Mhandisi Mativila alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Msumi Km 9.9 na daraja la Msumi na ujenzi wa barabara ya Goba Wakorea km 7.76 zilizopo Ubungo pamoja na ujenzi wa barabara ya Mivumoni Km 4.79 iliyopo Kinondoni ambapo utekele...