Posts

Showing posts from June, 2026

WAIRAQ WAFANYA YAO, WAKEMEA LAANA YA KUWAUA MABINTI MIAKA YA ZAMANI.*

Image
Jamii ya Kabila la Wairaq wanaoishi mikoa ya Arusha na Manyara mwishoni mwa wiki iliyopita walifanya sherehe kubwa ikiwemo dua na sala maalum na kukemea laana iliyofanywa na wazee wao karne kadhaa zilizopita za kuwaua watoto wa kike waliopata ujauzito nje ya ndoa. Tukio hilo kubwa lilifanyika jumamosi iliyopita katika makumbusho ya Urithi Geopark mjini Karatu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daniel Sillo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye. Viongozi wa kutoka kabila hilo walipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na watoto wa kike ambao kwa miaka sasa wamekuwa na maendeleo makubwa kiuchumi, kielimu na kisiasa na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwaendeleza wanawake ambao wana mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa. Naibu spika wa Bunge  Mhe. Sillo aliwataka wananchi wa kabila hilo kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujiletea maendeleo sambamba na kulinda amani ya taifa. Tukio hilo lilitangu...

*TANZANIA YAVUTIA UWEKEZAJI WA UJENZI WA VIWANDA VYA KUZALISHA BIDHAA ZA MIGODINI*

Image
▪️Waziri Mavunde akutana na Mwekezaji wa Kiwanda cha Kuzalisha Goroli za Chuma ▪️Ni kiwanda cha Oriental Casting and Forging Ltd cha China ▪️Kiwanda kikubwa kujengwa Buzwagi Kahama ▪️Tanzania yajipanga kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa za migodini Afrika 📍 Dar es salaam Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Juni 30, 2026 amekutana na Mkurugenzi Mkuu na Mmiliki wa Kiwanda cha Kuzalisha Goroli za Chuma “Steel balls” Bw. Hou Songcun kujadiliana juu ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini ili kuzalisha bidhaa za migodini. Waziri Mavunde amewakaribisha wawekezaji wao kwenye eneo lililotengwa na serikali la Buzwagi Special Economic Zone lililopo wilayani Kahama,Shinyanga kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bidhaa za migodini ili kuwahudumia wachimbaji wakubwa na wadogo nchini. Waziri Mavunde amesema serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu imejipanga kuhakikisha inavutia uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa bidhaa za migodini ili Tanzania kuwa kit...

*UKARABATI WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA HALE WAFIKIA ASILIMIA 83 YA UTEKELEZAJI*

Image
📌 Waziri Ndejembi amtaka mkandarasi kukamilisha ukarabati kwa wakati bila kuongezewa muda wa mkataba 📌 Kukamilika kwake  kutaongeza ufanisi wa uzalishaji na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani Na Mwandishi Wetu, Korogwe – Tanga Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini, huku Mradi wa Ukarabati wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale wilayani Korogwe, mkoani Tanga, ukifikia asilimia 83 ya utekelezaji. Akikagua maendeleo ya Mradi huo tarehe 29 Juni, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa, akisisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuongeza muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo. Waziri Ndejembi amesema kukamilika kwa ukarabati wa Kituo cha Hale kutaimarisha ufanisi wa uzalishaji wa umeme, kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Tanga na maeneo ya ...

DKT. KIJAJI AELEKEZA MAAFISA UHIFADHI KUHAKIKISHA MAENEO YA HIFADHI YANALINDWA NA KUHIFADHIWA

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewaelekeza maafisa uhifadhi nchini kuhakikisha maeneo yote ya hifadhi yanalindwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao kilichowakutanisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha, Wakuu wa Wilaya wa mkoa huo, watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo viongozi kutoka  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).  Kikao hicho kilijadili ongezeko la uvamizi na uharibifu wa misitu unaofanywa na watu mbalimbali katika maeneo ya hifadhi, hali inayohatarisha rasilimali za misitu na wanyamapori pamoja na juhudi za Serikali katika usimamizi endelevu wa maliasili. Katika kikao hicho, Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa maazimio yote yaliyofikiwa katika kikao hicho yanapaswa kutekelezwa kikamilifu na kwa wakati, akieleza kuwa hakuna nafasi ...

DKT MUNISI: PROGRAMU YA TAIFA YA UKUZAJI UJUZI YAENDELEA KUWAJENGA VIJANA

Image
✅VIJANA 5,746 WANUFAIKA NCHINI Na: Mwandishi Wetu - Mwanza Serikali imeendelea kudhihirisha dhamira thabiti ya kuwawezesha vijana kiujuzi kupitia Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi amesema hayo leo Juni 29, 2026 Mwanza alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema FDC kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo ya Uanagenzi yanayotolewa kupitia programu hiyo. Amesema, Serikali inalenga kujenga nguvukazi yenye ujuzi, maarifa na ubunifu ili kukidhi mahitaji ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuongeza ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Dkt. Munisi alisema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inaendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mfumo wa ubia (PPP), huku mafunzo ya uanagenzi yakichukua nafasi muhimu katika kuziba pengo la ujuzi kwa vijana.  Vile vile, amesema kuwa mfumo huo unamwezesha...

GRIDI YA TAIFA KUIMARISHWA KUPITIA MIRADI YA KIMKAKATI YA USAFIRISHAJI UMEME

Image
📌 Waziri Ndejembi aagiza kamati ya uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu katika Gridi ya Umeme ya Taifa  📌 Asisitiza kukamilika kwa miradi ya njia za kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 ili kuongeza uthabiti wa Gridi ya Taifa Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam  Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha Gridi ya Taifa kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya njia za.  kusafirisha umeme, inayotarajiwa kuongeza uwezo, uthabiti na usalama wa mfumo wa umeme nchini. Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Kituo cha Usimamizi wa Mfumo wa Gridi ya Taifa jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), amesisitiza umuhimu wa kukamilisha kwa wakati miradi ya njia za kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400, ikiwemo Chalinze–Kinyerezi na Chalinze–Dodoma, akieleza kuwa ndiyo msingi wa kuendelea kuimarisha Gridi ya Taifa na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na sekta za uzalishaji. “Kukamilika kwa miradi ya njia...

MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA MIRADI YA BILIONI 2.159 SAME

Image
Na Ashrack Miraji  SAME, Kilimanjaro, Juni 28 — Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Wazo Mwang'onda, ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.159 iliyotembelewa katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2026. Mwenge wa Uhuru uliwasili mkoani Kilimanjaro leo ukitokea Mkoa wa Tanga na kupokewa katika Kata ya Hedaru, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, alimkabidhi Mwenge huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Godfrey Mzava, kwa ajili ya kuendelea na mbio zake ndani ya wilaya hiyo. Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Godfrey Mzava alisema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 76 katika Wilaya ya Same na utapitia miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya Shilingi bilioni 2.159 kwa ajili ya kukaguliwa, kuwekwa mawe ya msingi, kuzinduliwa na kutembelewa. Katika ziara hiyo, Mwenge wa Uhuru ulikagua miradi ya afya, miundombinu, miradi ya kijamii, vikund...

*NGORONGORO NI NYUMBANI-WABUNGE*

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi kutoka Zanzibar wametembelea hifadhi ya Ngorongoro na kustaajabishwa na historia  ya binadamu, malikale, Urithi wa Utamaduni na Wanyamapori na kutoa wito kwa watu mbalimbali kutembelea hifadhi hiyo yenye hadhi tatu za Kimataifa zinazotambuliwa na UNESCO  Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao mbunge wa viti maalum Mhe. Zainab Abdallah   ameeleza kuwa katika ziara hiyo wameshuhudia maendeleo yaliyotukuka kuhusu uhifadhi, utalii, Malikale, urithi wa utamaduni na maendeleo ya jamii ambapo vinadhihirisha  kuwa Ngorongoro ni kivutio bora cha Utalii Barani Afrika. “Kuona ni kuamini, jana na leo tumetembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro na tumeona maendeleo makubwa yakifanyika na kwa macho yetu tumeshuhudia idadi kubwa ya watalii waliojawa na nyuso za bashasha na furaha kwa kushuhudia vivutio vilivyopo, mandhari na hali ya hewa ambayo unaipata Ngorongoro pekee”,amesema Mhe. Zainab. Wabunge k...

MTAKUWWA YAZINDUA KAMPENI Ya 'AMSHA ARI' MIRONGO KUHAMASISHA KUPINGA UKATILII KWA WANAWAKE NA WATOTO

Image
  Mwanza. Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto Mkoa wa Mwanza (MTAKUWWA) imezindua kampeni ya Amsha Ari katika Kata ya Mirongo, ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika malezi bora ya watoto, kuzuia mmomonyoko wa maadili na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Uzinduzi wa kampeni hiyo uliwashirikisha waendesha bodaboda wa Kata ya Mirongo, ambao walieleza utayari wao wa kushiriki kikamilifu katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuhamasisha ulinzi wa makundi hayo. Aidha, waendesha bodaboda hao waliitaka jamii kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini na kuwahimiza vijana kuepuka kutumika katika vitendo vya uchochezi vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti Mwenza wa MTAKUWWA Mkoa wa Mwanza, Yassin Ally, aliwataka waendesha bodaboda kuwa mstari wa mbele katika kufichua vitendo vya ukatili, kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari zake ...

RAIS DKT.SAMIA S. HASSAN KUFUNGUA MKUTANO MKUBWA WA MADINI NOVEMBA 2026*

Image
-▪️Ni Mkutano mkubwa wa Madini na Uwekezaji ▪️Washiriki 2000 kutoka mataifa 50 Duniani kushiriki ▪️Kauli Mbiu ya Mkutano inalenga kuongeza thamani madini kwa maendelezo ya Viwanda ▪️Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kuandaa mkutano huo ▪️Waziri Mavunde azindua rasmi maandalizi ya mkutano huo 📍 DAR ES SALAAM.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia S. Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Mkutano wa Saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC 2026) utakaofanyika Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Akizungumza leo Juni 27, 2026 wakati wa uzinduzi wa TMIC 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda unaotokana na madini kwa kuwekeza katika uchakataji na uyeyushaji wa madini badala ya kuendelea kuuza malighafi. Amesema kaulimbiu ya mkutano huo, "Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi," inaakisi dira ya serikali ya kui...

*MHE. SALOME AHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUPITIA MARATHON*

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, leo Juni 27, 2026 ameshiriki Mbio za Nishati Safi ya Kupikia (Clean Cooking Marathon) zilizofanyika katika Viwanja vya St. Peters Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza wakati wa kufungua mbio hizo, Mhe. Salome amesema pamoja na hatua nzuri iliyofikiwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini bado yako katika kiwango cha asilimia 28.6, hali inayoonesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia lengo la asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Amesema mbio hizo si mashindano ya kawaida ya kutafuta medali au vikombe, bali ni chachu ya mabadiliko ya kifikra na kijamii yanayolenga kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kuwawezesha wananchi kiuchumi, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034 unaolenga kuhakikish...