RC MTANDA AWATAKA MISUNGWI DC KUSHIRIKIANA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameitaka halmashauri ya wilaya ya Misungwi kuimarisha umoja baina ya Baraza la Madiwani na Menejimenti kuwaletea wananchi huduma bora za kijamii kwa kutumia mapato ya ndani kwa kujenga shule, vituo vya afya na miundombinu ya maji.

Mhe. Mtanda amefikia hatua ya kutoa agizo hilo baada ya kubaini uwajibikaji duni kwenye ukusanyaji kwa mwenendo wa miaka mitatu na udhaifu kwenye kujibu hoja ambapo kwa mwaka husika wa fedha hoja 81 zimetekelezwa 23 pekee sawa na asilimia 28.4 huku hoja 57 bado hazijajobiwa sawa na asilimia 70.4.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 24 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25 ambapo wamepata hati safi.

"Maendeleo ya Misungwi yanawategemea ninyi viongozi na watendaji mlioaminiwa hapa, mkileta mzaha kwenye uwajibikaji mtasababisha halmashauri hii kudumaa kiuchumi na wananchi wake kuishi maisha ya chini kwa kukosa huduma muhimu za kijamii." Mhe. Mtanda.

Aidha, Mhe. Mtanda ameonesha kukerwa na mwenendo mbovu wa mahudhurio ya wanafunzi shuleni kwani wanafunzi 613 hawajaripoti shuleni mpaka sasa kwenye usajili wa mwezi januari mwaka huu jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu.

Vilevile, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameonesha kusikitishwa na utokamilika kwa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo jambo ambalo linakwamisha juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi kwani miradi inaishia njiani.




 

>

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO