SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA WILAYA KUIMARISHA UCHUMI: MSIGWA




#Ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali-Mtumba Wafikia 95%

Mwanza

Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini kwa kupunguza barabara za changarawe na kujenga barabara za lami katika wilaya mbalimbali, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi kupitia shughuli za usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipokuwa akizungumza na Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaoendelea jijini Mwanza.

Msigwa amesema maofisa Mawasiliano wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya manufaa kwa wananchi wenyewe.

“Sisi ndiyo tunaobeba taswira ya Serikali. Tunapaswa kuwaonesha wananchi fursa zilizopo kutokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu unaofanywa na Serikali,” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali imejenga barabara za mzunguko zenye urefu wa kilomita 56 katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 95 kukamilika.

Aidha, amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara nyingine za mzunguko zinazounganisha Chamwino na maeneo mbalimbali jijini Dodoma kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri.

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO