WAFANYABIASHARA WAONGEZE USAHIHI: RISITI KILA UNUNUZI

WAFANYABIASHARA WAONGEZE USAHIHI: RISITI KILA UNUNUZI

Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX 

Na Musa Mathias
Kipeo Online Media 

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, amewataka wafanyabiashara kuendelea kutumia mashine za kielektroniki za kodi (EFD) na kuhakikisha kila mteja anapata risiti halali. Lengo kuu ni kupunguza mianya ya upotevu wa mapato ya serikali.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya,  Kasilda alisisitiza kuwa ni jukumu la kila mfanyabiashara kutoa risiti kwa kila mauzo anayofanya, huku akiwaasa wateja kudai risiti wanaponunua bidhaa.


“Tunatakiwa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara kutumia mashine za EFD, kutoa risiti kwa wateja huku wateja wakisisitizwa kudai risiti wanaponunua bidhaa, ili kulinda mapato ya serikali yasipotee,” alisema Kasilda.

​Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Same, Eliapenda Mwanri, alieleza kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 8.1 kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, ambapo lengo lilikuwa bilioni 8.04. Hii imesababisha kufanikiwa ukusanyaji wa asilimia 100.7 na kuvuka lengo lililowekwa.

Bw. ​Mwanri aliongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na utoaji wa elimu kwa walipakodi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, msisitizo wa matumizi ya risiti za kielektroniki kupitia mashine za EFD, kuimarika kwa ulipaji kodi kwa hiari, pamoja na utatuzi wa changamoto za walipakodi kwa wakati.

​Mkuu wa Wilaya hiyo bi. Kasilda, aliipongeza TRA Wilaya ya Same kwa jitihada hizo na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwawekea mazingira wezeshi sekta binafsi ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kikao hicho ni cha kisheria hufanyika mara mbili kwa mwaka ikiwa na lengo la kuangalia mwenendo wa makusanyo ya mapato katika wilaya na kushauri mikakati na namna ya kukusanya mapatoili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanatimia.






#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, 

Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX karibu sana.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO