Posts

Showing posts from December, 2025

MENEJA WA LUSHOTO EXECUTIVE LODGE AELEZA UZURI WA UTALII WA USANBARA LUSHOTO.

Image
 Meneja wa Lushoto Executive Lodge, Bw. Sifa Mwambire, amewakaribisha wageni wa ndani na nje ya nchi kutembelea wilaya ya Lushoto na kufurahia huduma bora pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika eneo hilo lenye mandhari ya kipekee. Akizungumza hivi karibuni, Bw. Mwambire alisema kuwa Lushoto Executive Lodge imejipambanua kwa kutoa huduma za kiwango cha juu katika mazingira tulivu na salama, huku ikilenga kuwahakikishia wageni faraja, ukarimu na mapumziko yenye ubora. Alisema lodge hiyo ni mahali sahihi kwa wageni wanaotafuta utulivu na huduma bora za malazi. Bw. Mwambire, ambaye pia ni mmoja wa wadau na wadhamini wakubwa wa walkathon iliyofanyika Magamba wilayani Lushoto, alisema ushiriki wao katika kudhamini tukio hilo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kukuza utalii na kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya hiyo. Alibainisha kuwa Lushoto imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo milima ya Usambara, misitu ya asili, maporomoko...

MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA AJIRA KWA WATANZANIA**

Image
📌*Ni Kupitia uzalishaji wa mkaa mbadala na teknolojia rafiki kwa mazingira* 📌*Wadau wahimizwa kushirikiana na TBS kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango* Imeelezwa kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yameendelea kufungua fursa nyingi za ajira kwa Watanzania, hususani katika uzalishaji wa mkaa mbadala na utengenezaji wa mashine za kuzalishia mkaa huo.  Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Nolasco Mlay amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Wazalendo Movement inayojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kuzalisha mkaa mbadala pamoja na uzalishaji wa mkaa huo wilayani Mkuranga mkoani Pwani. Bw. Mlay amesema kuwa taasisi nyingi zinazohudumia watu kuanzia 100 na kuendelea zimeanza kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, jambo linaloongeza kwa kiasi kikubwa mahitaji ya mkaa mbadala na hivyo kuhitaji uzalishaji wa kasi zaidi. “Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuzalisha mkaa mbadala pamoja na mitambo ya kute...

KUELEKEA MWAKA MPYA 2026,REA YAWASHIKA MKONO WAHITAJI*

Image
📍Hombolo - Dodoma Kuelekea Mwaka Mpya 2026, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewagusa Watanzania wenye mahitaji mbalimbali kwa kutoa mkono wa faraja na kuwatakia heri ya mwaka Mpya ujao. Zoezi la kuwapatia mahitaji walemavu limeongozwa na Bi. Judith Abdalah kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA mha. Hassan Saidy ambapo REA imetoa mahitaji mbalimbali kwa Kikundi cha Walemavu wa Ukoma waliopo Kata ya Hombolo jijini Dodoma.  Akiwasilisha salamu za REA, Bi. Abdalah amewataka walemavu wa Ukoma kuishi kwa upendo na amani na kusisitiza kuwa, REA itaendelea kuwashika mkono kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ili wakue kiuchumi na kijamii.  Halikadhalika, Swalehe Kibwana Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la REA (TUGHE), amesema zoezi hilo la kuwafikia na kuwasaidia wahitaji mbalimbali ni endelevu na REA itaendelea kutoa mahitaji kwao hususan kwa walemavu wa ukoma waliopo Hombolo.  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia mkoa wa Dodoma Bi. Fatuma Madudu a...

WIZARA YA AFYA YATOA ONYO KALI KWA WALE WANAOTUMIA JINA LA WAZIRI WA AFYA MHE MCHENGERWA KUTAPELI WATU

Image

TAHARIFA ZA KUREJEA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA UMEME

Image

MAKAMU WA RAIS DKT EMMANUEL NCHIMBI AUNGANA NA WAUMINI MBALIMBALI KWENYE MISA TAKATIFU YA NOEL

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameungana na Waumini mbalimbali katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Noeli (Krismasi), iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro, Osterbay Jijini Dar es Salaam. Tarehe 25 Desemba 2025.  

ROCK BLOCKS YADHAMINI ROMBO MARATHON, AKIELEZA MAFANIKIO NA MCHANGO KWA JAMII.

Image
ROCK BLOCKS YADHAMINI ROMBO MARATHON,  AKIELEZA MAFANIKIO NA MCHANGO KWA JAMII.  Rombo, Kilimanjaro.  Kampuni ya Rock Blocks imeeleza kufurahishwa kwake na mafanikio ya mashindano ya Rombo Marathon, yaliyofanyika katika viwanja vya Rongai, Wilayani Rombo, ambapo kampuni hiyo ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo. Akizungumza mara baada ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Rock Blocks, Fabian Oisso, amesema kuwa mbio za mwaka huu zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita, jambo linaloonesha kukua kwa tukio hilo na mwamko wa jamii kushiriki michezo. Amesema Rock Blocks ni kampuni inayojishughulisha na uchongaji wa miamba na kuzalisha bidhaa kuu tano za ujenzi, zikiwemo tofali za miamba na vigae, ambapo bidhaa zote hutengenezwa kwa kutumia miamba kwa asilimia 100. Oisso ameeleza kuwa kampuni hiyo imeamua kudhamini Rombo Marathon kwa sababu mashindano hayo yanafanyika ndani ya Wilaya ya Rombo, eneo ambalo pia ndilo makao ya mradi wa Rock Blocks. “Tuna...

BALOZI KOMBO AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS DKT SAMIA KWA KWA SULTAN HAITHAM BIN TARIQ WA OMAN

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Sultan  Haitham bin Tariq Al Said wa Oman. Akiwasilisha ujumbe  wamejadili kuhusu masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Oman

NGORONGORO YATANGAZA VIVUTIO VYA UTALII KWA WASHIRIKI WA ROMBO MARATHON.*

Image
Na Mwandishi Wetu, Rombo. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki katika tamasha la _Rombo _Marathon_ lililofanyika leo tarehe 23 Desemba 2025,  Rombo Mkoani Kilimanjaro na kuvutia wageni kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.  Ushiriki wa Ngorongoro Rombo Marathon ambayo pia watumishi wa Mamlaka hiyo wameshiriki mbio za umbali tofauti inadhihirisha jitihada za  mamlaka hiyo  kuunga mkono sekta ya michezo,  kutangaza vivutio vya utalii  kupitia utalii wa michezo, kujenga uhusiano na wadau kupitia matukio ya kijamii na kitaifa na kimataifa. Sambamba na kushiriki katika tamasha hilo, wananchi waliohudhuria mashindano hayo walipata fursa ya kutembelea banda la Ngorongoro lililowekwa mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu kwa washiriki na wananchi kwa ujumla kuhusu shughuli za Uhifadhi na utalii pamoja  na mchango wa hifadhi ya Ngorongoro katika kulinda urithi wa asili na wa kitamaduni.

RUSHWA YATAJWA KUHARIBU MFUMO WA UTOAJI HAKI*

Image
Rushwa imetajwa kuwa ni janga kubwa linaloharibu kwa kiwan go kikubwa mfumo mzima wa utoaji haki, hivyo kuhatarisha misingi ya haki, uwajibikaji na utawala bora. Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 23, 2025 na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Uchumi wa Madini na Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (Local content & CSR), Terrence Ngole, ambaye amemwakirisha  Katibu Mkuu Wizara ya Madini wakati akifungua mafunzo maalumu kwa Menejimenti ya Wizara ya Madini yanayolenga kujadili madhara ya rushwa pamoja na namna ambavyo rushwa inavyodhoofisha mfumo wa haki katika taasisi za umma. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Ngole amesema kuwa rushwa huathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa majukumu ya Serikali, hususan katika sekta nyeti kama utoaji wa haki, ambapo vitendo vya rushwa husababisha kukosekana kwa usawa, upendeleo na kupungua kwa imani ya wananchi kwa taasisi za umma. “Rushwa ni adui mkubwa wa haki. Inapopenya katika mifumo...

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA VITUO VYA VIJANA- OMOLO

Image
Na: OR-MV, Morogoro Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana Bi. Jenifa Omolo ameeleza  dhamira ya serikali katika kuvifanyia marekebisho vituo vya maendeleo ya vijana nchini ili viwe chachu ya kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kielimu. Katibu Mkuu huyo amefanya ukaguzi huo leo (23 Desemba 2025) katika kituo cha Ilonga wilaya ya Kilosa  na kusisitiza kuwa vituo hivyo vya maendeleo ya vijana vina manufaa makubwa kwa vijana katika kuwajengea ujuzi wa vitendo. “Kituo hiki cha Ilonga kilichopo Morogoro ni moja ya vituo vitatu (3) ambavyo ni cha Sasanda - Songwe na Marangu kilichopo Kilimanjaro ambapo amesema vituo hivyo viko kwenye mpango mkakati wa kuboreshwa ili viwasaidie vijana wanaoishi karibu na maeneo ya vituo hivo na kuendana na teknolojia” amesema. Katika hatua nyingine Omolo amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya Maendeleo ya Vijana nchin...

SERIKALI YASISITIZA USALAMA , MAPATO MPAKANI MUTUKULA

Image
Na Mwandishi Wetu,KAGERA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amehimiza ushirikiano kati ya  watumishi wa serikali waliopo katika Kituo cha Forodha cha Pamoja cha Mutukula kilichopo wilayani Misenyi mkoani Kagera ambapo ni mpaka kati ya nchi ya Tanzania na Uganda huku akiwaasa kutilia mkazo masuala ya usalama na ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya nchi ambapo uhitaji wa usalama na mapato ni muhimu ili nchi iweze kukua kiuchumi. Ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali za kiforodha katika kituo hicho  akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kagera ambapo awali alipowasili mkoani humo alipata ripoti ya hali ya ulinzi na usalama kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Hajjat Fatma Mwassa,ripoti iliyoonyesha kuwepo kwa sintofahamu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ikiwemo wingi wa vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu na watu wanaoweza kuingia nchini kwa nia ovu ya kuvuruga amani iliyopo. ‘Kwanza ni usalama wa nchi yetu, kw...

SANGU ATAKA WAAJIRI KUSAJILI MAENEO YAO YA KAZI OSHA

Image
Na: OWM - KAM, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanasajili maeneo yao ya kazi OSHA ili kutekeleza taratibu za usalama na afya kwa mujibu wa Sheria. Sangu ametaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waajiri watakaobainika kutosajili maeneo yao. Sangu ametoa kauli hiyo leo Disemba 22, 2025 alipotembelea Ofisi za Wakala wa Usalama na  Afya Mahali pa Kazi (OSHA), JijiniDar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli zinazotekelezwa na taasisi hiyo. Vilevile, Waziri Sangu ameigiza OSHA  kufanya kampeni maalumu ya usajili nchi nzima ili waajiri wazingatie viwango vya usalama na afya, hivyo kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi. Kwa upande mwengine, Waziri huyo  ametoa rai kwa menejimenti na watumishi wa OSHA kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatoa huduma bora, kufanya kaguzi na kushauri namna bora ya kuandaa na kusimika mifumo itakayowezesha ku...

SERIKALI KUJENGA MTAMBO WA KUCHENJUA DHAHABU MWAKITOLYO SHINYANGA*

Image
■ Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ▪️Zaidi ya tani 100 - 120 kuchenjuliwa kwa siku ■ Makundi ya vijana na wanawake kupatiwa leseni kupitia programu ya MBT ■ Leseni zisizoendelezwa kufutwa kwa mujibu wa sheria ■ Aelekeza Wachimbaji kufuata kanuni za usalama za uchimbaji kuepuka madhara *Mwakitolyo, Shinyanga Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* ya kuwasimamia wachimbaji wadogo, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ipo mbioni kuanza ujenzi wa mtambo wa kuchenjua madini ya dhahabu mkoani Shinyanga. Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Desemba, 2025 na Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde* alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na wachimbaji katika eneo la Mwakitolyo lililopo Shinyanga Vijijini. Waziri Mavunde alitangaza habari hizo njema kuwa, tayari Shirika la STAMICO limeanza utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais na kwamba eneo limeshapatikana katika Kijiji cha Mawemelu na ujenzi utaanza hivi karibuni. ...

DC SUMAYE: MAGAMBA WALKATHON NI FURSA YA KUKUZA UTALII LUSHOTO

Image
Na Ashrack Miraji  MKUU wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Zephania Sumaye ameipongeza Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba wilayani Lushoto kwa kuandaa Magamba Walkathon ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo wilayani Lushoto ikiwemo hifadhi hiyo.  Sumaye aliyasema hayo mara baada ya kushiriki mbio hizo wiki hii ambazo zilikuwa za kilomite 20,10 na 5 huku akieleza matukio kama hayo yanasaidia kuwaweka pamoja na kusaidia kujenga afya na mahusiano kwa jamii mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo na maeneo mengine hapa nchini. “Tunapoelekea kufunga mwaka matukio kama hayo yanatuleta pamoja na kutusahaulisha na matatizo yao na kujenga afya na kuwaimarisha leo hii nimesimama hapa Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Balozi Batilda Burian ametuma salamu nyingi na kupongeza matembezi haya ambayo yamekuwa na muendelezo kwa kipindi cha miaka mitatu”Alisema  Alisema kwamba anaamini mwakani watafaya kitu kiubwa zaidi ili kuweza kuwavuta watu wengi...