SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA VITUO VYA VIJANA- OMOLO
Na: OR-MV, Morogoro
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana Bi. Jenifa Omolo ameeleza dhamira ya serikali katika kuvifanyia marekebisho vituo vya maendeleo ya vijana nchini ili viwe chachu ya kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kielimu.
Katibu Mkuu huyo amefanya ukaguzi huo leo (23 Desemba 2025) katika kituo cha Ilonga wilaya ya Kilosa na kusisitiza kuwa vituo hivyo vya maendeleo ya vijana vina manufaa makubwa kwa vijana katika kuwajengea ujuzi wa vitendo.
“Kituo hiki cha Ilonga kilichopo Morogoro ni moja ya vituo vitatu (3) ambavyo ni cha Sasanda - Songwe na Marangu kilichopo Kilimanjaro ambapo amesema vituo hivyo viko kwenye mpango mkakati wa kuboreshwa ili viwasaidie vijana wanaoishi karibu na maeneo ya vituo hivo na kuendana na teknolojia” amesema.
Katika hatua nyingine Omolo amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya Maendeleo ya Vijana nchini hatua iliyopelekea kuanzishwa Wizara ya Vijana.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameishukuru Wizara hiyo kwa kuwa na mpango mkakati wa kufufua vituo vya Maendeleo ya Vijana wilayani hapo na kuahidi kuwa Ofisi yake itaonyesha ushirikiano thabiti ili kufanikisha Malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa wananchi wanaoishi karibu na kituo cha hicho Bi. Mariam Saidi wamefurahishwa kuona ujio wa Katibu Mkuu na wameishukuru serikali kwa mpango mkakati wake wa kuboresha kituo hicho kwa ustawi wa maendeleo ya vijana.







Comments
Post a Comment