ROCK BLOCKS YADHAMINI ROMBO MARATHON, AKIELEZA MAFANIKIO NA MCHANGO KWA JAMII.
ROCK BLOCKS YADHAMINI ROMBO MARATHON, AKIELEZA MAFANIKIO NA MCHANGO KWA JAMII.
Rombo, Kilimanjaro.
Kampuni ya Rock Blocks imeeleza kufurahishwa kwake na mafanikio ya mashindano ya Rombo Marathon, yaliyofanyika katika viwanja vya Rongai, Wilayani Rombo, ambapo kampuni hiyo ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo.
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Rock Blocks, Fabian Oisso, amesema kuwa mbio za mwaka huu zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita, jambo linaloonesha kukua kwa tukio hilo na mwamko wa jamii kushiriki michezo.
Amesema Rock Blocks ni kampuni inayojishughulisha na uchongaji wa miamba na kuzalisha bidhaa kuu tano za ujenzi, zikiwemo tofali za miamba na vigae, ambapo bidhaa zote hutengenezwa kwa kutumia miamba kwa asilimia 100.
Oisso ameeleza kuwa kampuni hiyo imeamua kudhamini Rombo Marathon kwa sababu mashindano hayo yanafanyika ndani ya Wilaya ya Rombo, eneo ambalo pia ndilo makao ya mradi wa Rock Blocks.
“Tuna kila sababu ya kufurahia na kuunga mkono mbio hizi kwa kuwa zinafanyika katika wilaya yetu, ambako pia mradi wetu unatekelezwa,” alisema Oisso.
Aidha, aliongeza kuwa kupitia Rock Blocks, kampuni imefanikiwa kutoa ajira kwa vijana, kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu, pamoja na kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira, kutokana na ukweli kwamba bidhaa zake zote zinatokana na miamba asilia kwa asilimia 100.
Kwa hatua hiyo, Rock Blocks inaendelea kuwa mfano wa kampuni inayochangia maendeleo ya michezo, ajira, uchumi wa ndani na uhifadhi wa mazingira katika Wilaya ya Rombo na Tanzania kwa ujumla.

Comments
Post a Comment