KAMISHNA BADRU ATOA KONGOLE KWA TIMU ZA NGORONGORO ZILIZOSHIRIKI SHIMMUTA*



Tarehe 5 Desemba, 2025 Morogoro.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Abdul-Razaq Badru amezipongeza timu za Mamlaka hiyo zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya serikali na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kuendelea kulinda na kutangaza taswira ya taasisi hiyo kupitia sekta ya Michezo.

Akitoa salamu  alipotembelea timu hiyo kwa niaba  Kamishna Badru, Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma bwana Hamis Dambaya amesema menejimenti ya Ngorongoro imeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na timu hizo katika mashindano hayo na kulitangaza shirika kupitia utalii wa michezo (sport tourism) 

Katika mashindano hayo Ngorongoro imefanikiwa kutwaa Medali saba huku ikidhihirisha upekee wake kimataifa na kuendelea kuwa _Premium Safari Destination._


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO