MAKAMU WA RAIS DKT EMMANUEL NCHIMBI AMEMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI NA (SADC)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa mpito wa SADC ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.

Aidha, Mkutano huo umepitisha mapendekezo mbalimbali ikiwa ni juhudi ya kuimarisha hali ya amani na usalama katika Jamhuri ya Madagascar na kutoa wito wa mazungumzo ya kitaifa yatakayopelekea uchaguzi huru wa kidemokrasia nchini humo.

Halikadhalika, Mkutano huo umeipitisha Jamhuri ya Zambia kuwa Mwenyekiti Ajaye wa Mpito wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.




Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO