DC RUKIA ATEMBELEA MIUNDOMBINU YA TANESCO NA SAMWASA
DC RUKIA ATEMBELEA MIUNDOMBINU
YA TANESCO NA SAMWASA.
Mwanga, Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Bi. Rukia Zuberi akiwa ameambatana na viongozi wengine ngazi ya wilaya, wamefanya ziara kwenye miundombinu ya umeme iliyo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Same-Mwanga (SAMWASA) kwa lengo la kuona hali halisi ya utendaji kazi, kujadili na kushauriana ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Akieleza lengo la ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya, Bi. Rukia Zuberi, amesema ni kuona hali halisi ya utendaji, kujadili na kushauriana namna ya kukabiliana changamoto zinazozikabili taasisi hizo, ili ziweze kuendelea kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.
Akiwa katika ofisi hizo, alipata maelezo kutoka kwa watumishi kuhusu mifumo ya kazi, utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta za umeme na maji, huku akielezwa juhudi zinazofanyika kuboresha huduma hizo.
Hata hivyo amesisitiza utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu kutunza na kulinda miundombinu ya maji na umeme ili iweze kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.
Aidha, Bi. Zuberi amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu, huku wakizingatia ushirikiano baina yao na wadau wengine ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, za uhakika na kwa wakati.
Kwa upande wao, taasisi hizo zimeshukuru kwa ziara hiyo, zikieleza kuwa imewapa motisha na fursa ya kujitathmini, huku zikiahidi kuendelea kuboresha huduma zao kwa lengo la kuondoa malalamiko ya watumiaji wa huduma zinazotolewa na taasisi hizo.
#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update
Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX





Comments
Post a Comment