USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA WAPEWA KIPAUMBELE SEKTA YA MADINI.



Na Deborah Lemmubi -Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde ameeleza kuwa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini umeendelea kupewa kipaumbele ambapo Wizara hiyo imefanya marekebisho ya kanuni ya Ushirikishwaji wa wazawa ya mwaka 2018 ambapo Tume ya Madini itatangaza kupitia kanuni ya 13A orodha ya bidhaa na huduma ambazo zinatakiwa kutolewa na kampuni za Kitanzania zinazomilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Januari 5,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kutoa Taarifa kwa Umma kuhusu maendeleo katika Sekta ya Madini. 

Na kuongeza kuwa malengo ya kufanya hivyo ni kuongeza wigo wa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini kwa manufaa mapana ya Taifa ambapo kwa awamu ya kwanza Novemba 14,2025 Tume ya Madini ilitangaza orodha ya bidhaa 20 na huduma zinazotakiwa kutolewa na kampuni hizo ikiwemo Supply of General Lubricant,Legal Services na Vehicle Hire.

 "Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya marekebisho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za mwaka 2018 ambapo Tume ya Madini mara kwa mara itatangaza kupitia Kanuni ya 13A orodha ya bidhaa na huduma ambazo zinatakiwa kutolewa na kampuni za Kitanzania ambazo zinamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania, lengo likiwa ni kuongeza wigo wa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini kwa manufaa mapana ya taifa".

" Kwa awamu ya kwanza tarehe 14 Novemba, 2025 Tume ya Madini ilitangaza orodha ya bidhaa na huduma zinazotakiwa kutolewa na kampuni zinazomilikiwa na kampuni za kitanzania kwa asilimia 100".

Aidha Waziri amesema kuwa katika kuendeleza Ushirikishwaji huo wa Watanzania,Tume ya Madini imeanzisha utaratibu wa kuendesha Majukwaa ya Utekelezaji wa Ushirikishwaji huo katika Sekta ya Madini kwa kila mwaka ambayo yanahusisha Wamiliki wa leseni, watoa huduma na wasambazaji bidhaa migodini,Taasisi mbalimbali za Serikali na Wizara na Taasisi zake lengo ikiwa ni kutathmini utekelezaji wa kanuni za ushirikishwaji wa watanzania.

" katika kufanikisha lengo la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kwa kufungamanisha Sekta ya Madini na Sekta nyingine za uchumi,Tume ya Madini imeanzisha utaratibu wa kuendesha Majukwaa ya Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kila mwaka ambayo yanahusisha Wamiliki wa leseni, watoa huduma na wasambazaji bidhaa migodini, Taasisi mbalimbali za Serikali, Wizara ya Madini na Taasisi zake, Lengo la majukwaa hayo ni kutathmini utekelezaji wa kanuni za ushirikishwaji wa Watanzania".

Waziri amesema katika miradi hiyo ya madini pia kumeshuhudiwa ongezeko la ajira kwa Watanzania kutoka ajira 6,668 kati ya ajira 7,003 ikiwa ni sawa na asilimia 95 kwa mwaka 2018 hadi kufikia ajira 18,853 kati ya ajira 19,356 sawa na asilimia 97 kufikia Desemba 2024.

 Na pia katika nafasi zinazohitaji kupata uzoefu kutokana na kukua kwa teknolojia duniani, kumekuwa na utaratibu wa Kisheria wa urithishwaji wa Watanzania kwa nafasi zinazoshikiliwa na Wataalamu wa Kigeni ikiwa ni kutimiza azma ya Serikali ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaoshikilia nafasi za uongozi katika Kampuni za uchimbaji mkubwa na wa kati wa madini.

Pamoja na hayo Waziri Mavunde ametumia Wasaa huo kutoa Rai kwa Watanzania kuendelea kuhakikisha wanapata utaalamu sahihi unaohitajika katika shughuli za madini ili kuweza kuwa miongoni mwa wanaostahili kupatiwa fursa za ajira katika migodi sambamba na fursa za utoaji huduma katika miradi hiyo.

Ikiwa ni pamoja watoa huduma wote kuhakikisha wanatoa huduma bora kulingana na viwango stahiki ili kuendelea kuaminika katika utoaji wa huduma husika.


Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO