WIZARA YA MAJI YAFUNGUA MILANGO KWA SEKTA BINAFSI KULETA MAGEUSZI SEKTA YA MAJI.
Na Deborah Lemmubi -Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema kuwa Wizara hiyo imefungua milango kwa wadau mbalimbali wa Sekta binafsi ili kushirikiana na Wizara katika huduma ya utoaji Maji na kufanya mageuzi kwa kuhakikisha vijiji 1575 ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji vinafikiwa na huduma hiyo na kuondokana na changamoto ya maji inayopatikana kwa baadhi ya vijiji.
Waziri Aweso ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Januari 28,2026 wakati akielezea mafanikio mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Wizara hiyo katika suku 100 za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na kusema ufungaji wa mita za malipo ya kabla nayo pia itachangia kupunguza changamoto zilizopo katika huduma maji ikiwemo ubambikiaji wa ankara na upotevu wa maji utatatuliwa kwa kutumia Teknolojia.
"Tumebadilisha Sera kwa maelekezo ya Mhe Rasi ambayo sasahivi Sera ya Wizara ya maji imeweza kuwakaribisha Sekta binafsi kuja kushirikiana pamoja nasi ili kufanya mageuzi katika Wizara ya maji".
Aidha Waziri Aweso amesema kuwa Wizara imejipanga vizuri kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya maji yaliyo safi,salama na toshelevu na kuhakikisha watumishi wake kutokuwa kikwazo katika kufanikisha na kufikia lengo.
"Pamoja na Wizara kujipanga vizuri lakini Rais wetu ni Mama hivyo hataki kusikia wala kuona kina Mama wa nchi hii wakiteseka kufuata huduma hiyo muhimu kwani anajua adha wanayopata akina Mama hao kutokana na ukosefu wa maji".
Pamoja na hayo Waziri amesema kuwa Wizara itatumia rasilimali zilizopo za vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji yanawafikia wananchi popote walipo kwani Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji ikiwemo maziwa makuu kama vile Ziwa Tanganyika na Ziwa Viktoria pamoja na uwepo wa mito mikuwa ikwemo mto Rufiji,Pangani na mingineyo.



Comments
Post a Comment