Posts

Showing posts from July, 2025

MFUMO WA BIASHARA YA MADINI TANZANIA WAIVUTIA UGANDA

Image
MFUMO WA BIASHARA YA MADINI TANZANIA WAIVUTIA UGANDA Na Mwandishi Wetu. Dodoma.  Wizara ya Madini na Fedha ya Jamhuri ya Uganda imeonesha kuvutiwa na namna Tanzania inavyoendesha shughuli za biashara ya madini, hususan mfumo wa masoko unaotumika nchini, ikilenga kuboresha mifumo yao kwa kutumia uzoefu wa Tanzania kama mfano wa mafanikio. Hayo yamebainishwa leo Julai 31, 2025 jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe kutoka Uganda uliofika katika Wizara ya Madini ya Tanzania ukiongozwa na Kamishna wa Madini wa Uganda Agnes Alabai kwa madhumuni ya kujifunza kuhusu mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa biashara ya madini pamoja na masoko ya madini nchini Tanzania. Pia, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kuwapatia mafunzo na taarifa mbalimbali zinazolenga kuboresha ufanisi wa sekta ya madini kwa kuzingatia uwazi bila kuficha taarifa yoyote. Alabai amesema ziara hiyo imekuwa ni sehemu ya juhudi za Uganda kuimarisha sekta yake ya madini kwa kuiga mifumo yenye mafanikio kutoka mataifa jirani. K...

NCAA YANOGESHA WORLD RANGERS DAY KWA KUFANYA MICHEZO NA SHUGHULI ZA KIJAMII KARATU

Image
Na Philomena Mbirika, Karatu Arusha. Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imehitimisha maadhimisho ya siku ya askari Wanyamapori duniani kwa kufanya michezo mbalimbali iliyohususu askari wa Jeshi la Uhifadhi, askari wa Jeshi la polisi wilaya ya Karatu pamoja na kufanya shughuli ya upandaji miti katika shule ya Sekondari Welwel iliyopo Karatu Mkoani Arusha. Kamishna wa Uhifadhi NCAA ameongoza maafisa na askari katika zoezi la kupanda miti Shule ya Sekondari Welweli, kutoa elimu ya shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa wanananchi na kuongoza watumishi hao katika michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia kilomita tano, mchezo wa mpira wa miguu kati ya askari wa jeshi la Uhifadhi kutoka pori lla akiba Pololeti, askari walioko eneo la hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Polisi Karatu. “NCAA ni sehemu ya Jamii, katika utekelezaji wa majukumu yetu tunashirikiana na vyombo vingine ikiwepo Polisi Wilaya za Ngorongoro na karatu pamoja na wananchi, ndio maana leo tumefanya michezo ya...

*RAIS SAMIA AIPA NEEMA MIRADI YA KUZALISHA UMEME IRINGA*

Image
*📌Atoa zaidi ya bilioni 15 mradi wa Mwenga Hydro Ltd* *📌Mwenga Hydro Ltd yaunganisha wateja 8,000 huduma ya umeme* 📍Mufindi - Iringa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  ametoa kiasi cha shilingi bilioni 15 kwenye mradi wa kuzalisha umeme wa Mwenga Hydro Ltd uliopo Wilaya ya mufindi mkoani Iringa. Hayo yamebainishwa leo Julai 31, 2025 wakati wa ziara ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ilipotembelea na kukagua mradi wa kuzalisha umeme wa Mwenga Hydro Ltd ambao unatumia nguvu ya maporomoko madogo ya maji (small hydro power potential) ya mto na upepo katika kuzalisha umeme.  Akizungumza katika ziara hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, Mjumbe wa Bodi, Bw. James Mabula ameeleza kuwa, Rais Samia ametoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kuwezesha utekelezaji na uzalishaji wa umeme mradi wa Mwenga mkoani humo.  "Kupitia fedha hizo zinaz...

ENDELEENI KULINDA RASILIMALI ZA WANYAMAPORI NA MISITU KWA WELEDI NA KUJITUMA-KAMISHNA BADRU*

Image
Kassim Nyaki, NCAA Kamishna wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Abdul-razaq Badru amewataka askari wa uhifadhi wa taasisi hiyo kuendelea kulinda rasilimali za wanyamapori, Misitu na malikale kwa ari na weledi ili taifa liendelee kunufaika na rasilimali hizo. Kamishna Badru ametoa maelekezo hiyo  katika kilele cha siku ya askari wanyamapori duniani  (World Rangers Day) leo tarehe 31 Julai, 2025 ambapo mamlaka hiyo imedhimisha siku hiyo katika viwanja vya mnadani Karatu Mkoani Arusha. Amesema mamlaka inatambua mchango wa askari wa uhifadhi kutokana na kujitoa kwao kulinda rasilimali hizo hivyo iko tayari kuboresha utendaji wao ili uendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutambua mchango huo imewapa vyeti na fedha kufuatia juhudi na kujitoa kwao katika ulinzi wa kupambana na vitendo vya ujangili hali iliyosaidia kuokoa rasilimali za wanyamapori, mali za shirika na askari wengine. “Maadhimisho haya ni maalum kwa ajili ya kutambua na kue...

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA BIL. 19 WILAYA YA TABORA

Image
Na Ashrack Miraji  Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 19.17 katika Wilaya ya Tabora, mkoani Tabora. Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ally Usi, aliwapongeza viongozi wa Wilaya ya Tabora kwa kusimamia kwa ufanisi miradi hiyo ambayo imeidhinishwa na Mwenge wa Uhuru kuizindua rasmi. “Uongozi wa Wilaya ya Tabora umeonyesha mfano wa kuigwa. Miradi hii imekidhi vigezo vya kitaifa na inaleta matumaini makubwa kwa wananchi,” alisema Usi. Katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mheshimiwa Thomas Myinga, alimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mheshimiwa Upendo Wella, kuendeleza mbio hizo ndani ya wilaya hiyo. Miradi iliyozinduliwa inahusisha sekta muhimu kama elimu, afya, maji, na miundombinu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na mikakati ya Serikali katika kuinua maisha ya wana...

WITO WATOLEWA KUUNGA MKONO USTAWI WA WATOTO YATIMA

Image
WITO WATOLEWA KUUNGA MKONO USTAWI WA WATOTO YATIMA. Na Mwandishi Wetu.  Dar Es Salaam. Jamii imeaswa kuwasaidia Watoto wenye changamoto mbalimbali wakiwemo Watoto yatima na wanaoishi na kufanya kazi mtaani ili waweze kupata Malezi Bora na mahitaji kama Watoto wengine. Wito huo umetolewa Julai 30, 2025 mkoani Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu alipotembelea Shirika la SOS Village. Dkt. Jingu amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha Watoto wenye changamoto mbalimbali wanapatiwa huduma stahiki ili nao wakue na kupata fursa sawa kama Watoto wengine. Ameongezea kuwa katika kuwasaidia Watoto hao Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la SOS Village ambalo limejikita katika kuwasaidia Watoto wenye changamoto mbalimbali kwa kuwapatia huduma stahiki katika Kijiji chao cha kulelea Watoto. "Nimetembelea nyumba ze...

KAMISHNA BADRU AWATAKA WATUMISHI KIMONDO CHA MBOZI KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII*

Image
Na Mwandishi wetu, Mbozi Songwe Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-razaq Badru amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo waliopo kituo cha Kimondo cha Mbozi mkoani Songwe kufanya kazi kwa ari kubwa na kujituma ili eneo hilo liweze kuwa kitega uchumi muhimu kwa maendeleo ya taifa. Kamishna Badru ametoa rai hiyo alipofanya  ziara ya kikazi na kuzungumza na watumishi wa  kituo hicho  na kusisitiza kuwa Serikali kupitia NCAA imefanya kazi kubwa ya kuboresha eneo hilo kwa kujenga jengo jipya la makumbusho ya kisasa na kuweka vioneshwa mbalimbali hasa vinavyohusu mila na desturi za makabila ya mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuvitangaza na kufanya eneo hilo kuwa kitega uchumi kizuri kwa maendeleo ya taifa. Aliwaeleza watumishi hao kuwa uwepo wao katika kituo hicho ni muhimu kwa kuwa NCAA  ina mipango ya kuboresha zaidi mazingira ya hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea na kufanya eneo hilo kuwa chanzo kizuri cha ...

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MKUTANO WA ACTIF 2025 NCHINI GRENADA*

Image
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Julai 27, 2025 amewasili mjini St. George’s, nchini Grenada ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la nne wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum - ACTIF 2025) unaotarajiwa kufanyika Julai 28–30, 2025 katika kituo cha mikutano cha Radisson. Mkutano huo mkubwa unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na visiwa vya Karibiani una kaulimbiu inayosema: _“Uhimilivu na Mabadiliko: Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Afrika na Karibiani katika Kipindi cha Changamoto za Kidunia.”_ Katika mkutano huo, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki mjadala wa Mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali, kukutana na viongozi wa mataifa mengine, pamoja na kushiriki katika mikutano ya uwili na wawekezaji wakubwa, ikiwa ni dhamira ya Tanzania ya kuendeleza juhudi zake za kuvutia wawekezaji wa kimataifa ili kusaidia katika kujenga uchumi wa kisasa na shindani duniani. Ushir...

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI BALOZI MAHMOUD KOMBO AKUTA NA RAIS WA JAMHURI YA RWANDA MHE PAUL KAGAME

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, Ikulu ya Kigali, Rwanda. Viongozi hao wameangazia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda pamoja na matunda  Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda, uliofanyika kwa siku tatu jijini Kigali, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Julai, 2025.  

WAZIRI KOMBO ATAKA MIKAKATI ENDELEVU YA KISEKTA KUIMARISHA MIFUMO YA CHAKULA KIMATAIFA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti na za pamoja katika kuimarisha mifumo ya chakula ili kuhakikisha ushiriki endelevu wa Tanzania katika ajenda za maendeleo ya kimataifa.  Waziri Kombo ameyasema hayo wakati wa kikao kilichofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini Addis Ababa, Ethiopia, ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (UNFSS+4), unaofanyika tarehe 27 hadi 29 Julai 2025. Wakati wa kikao hicho, Waziri Kombo amepokea taarifa kuhusu maandalizi ya mkutano kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo ambaye ameeleza kuwa mkutano huo ni jukwaa la kipekee kwa Tanzania kushiriki katika kujenga ajenda ya kimataifa ya kilimo, kukuza usalama wa chakula, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Id...