TANZANIA NA MAREKANI ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KISEKTA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo, alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Andrew Lentz, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

Mazungumzo hayo, yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika maeneo ya maslahi ya pamoja.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Ndani, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji pamoja na maafisa waandamizi wengine kutoka Serikalini.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO