MABONDIA TANZANIA KUNOGESHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA COMORO*
Mabondia wanne wa Tanzania wakiambatana na makocha wao ni miongoni mabondia walioalikwa kunogesha maadhimisho ya miaks 50 ya Uhuru wa Comoro ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Mabondia hao Kassim Mbundwike na Ezra Mwanjango wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Kaimu Kaimu na Samuel Kapungu kutoka Shirikisho la Ngumi za Ridhaa watachuana na Mabondia kutoka Madagascar,Reunion na wenyeji Comoro kama sehemu ya Maadhimisho hayo na walipata wasaa wa kutembelea Ubalozi wa Tanzania kwa kuratibiwa na Mwambata Jeshi,Kanali Abdulrahim
Mahmoud Abdallah.
Awali akitoa maelezo ya ziara hiyo,kiongozi wa msafara huo Valerian Lugongo alieleza kuwa wamejipanga vyema na wana imani ba ushindi.
Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini humo akiwakabidhi Bendera ya Taifa alieleza kuwa Sherehe hizo ni tukio kubwa kuwahi kutokea miaka ya karibuni na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye atashiriki maadhimisho hayo atapata faraja kubwa kupata habari njema za ushindi.
Comments
Post a Comment