KAMISHNA BADRU AWATAKA WATUMISHI KIMONDO CHA MBOZI KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII*


Na Mwandishi wetu, Mbozi Songwe

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-razaq Badru amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo waliopo kituo cha Kimondo cha Mbozi mkoani Songwe kufanya kazi kwa ari kubwa na kujituma ili eneo hilo liweze kuwa kitega uchumi muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Kamishna Badru ametoa rai hiyo alipofanya  ziara ya kikazi na kuzungumza na watumishi wa  kituo hicho  na kusisitiza kuwa Serikali kupitia NCAA imefanya kazi kubwa ya kuboresha eneo hilo kwa kujenga jengo jipya la makumbusho ya kisasa na kuweka vioneshwa mbalimbali hasa vinavyohusu mila na desturi za makabila ya mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuvitangaza na kufanya eneo hilo kuwa kitega uchumi kizuri kwa maendeleo ya taifa.

Aliwaeleza watumishi hao kuwa uwepo wao katika kituo hicho ni muhimu kwa kuwa NCAA  ina mipango ya kuboresha zaidi mazingira ya hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea na kufanya eneo hilo kuwa chanzo kizuri cha mapato kwa Serikali.


Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Kimondo cha Mbozi Afisa Uhifadhi Mwandamizi Andrew Lowasa amemweleza kamishna wa Uhifadhi kuwa kituo hicho katika mwaka wa fedha 2024/2025 kimetembelewa na wageni  2,525 kutoka ndani na nje ya nchi 

Kamishna wa Uhifadhi NCAA Abdul-razak Badru yupo kwenye ziara ya kuvitembelea vituo mbalimbali vya urithi wa utamaduni na Mambokale  vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo nje ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kukagua utendaji kazi katika maeneo hayo.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO