DKT. JINGU ATOA WITO KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI MISUNGWI KUWA MABALOZI WA MAENDELEO KATIKA JAMII. ‎


Na WMJJWM – Mwanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amewataka wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi Mwanza, kuwa mabalozi wa maendeleo katika jamii kwa kutumia maarifa na ujuzi walioupata chuoni humo.

Akizungumza na wanafunzi hao Julai 04, 2025 Dkt. Jingu amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kutumia elimu yao si tu kwa kujikwamua kiuchumi, bali pia kuwa mfano wa maadili mema katika jamii zao. Amehimiza vijana hao kushiriki kikamilifu katika fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ikiwemo fursa ya ununuzi wa umma ya asilimia 30 kwa makundi maalum. 

“Ninawaomba mkawe mabalozi wazuri wa maendeleo katika jamii zenu mkafanye yale yote mazuri mliyofundishwa hapa chuoni na kuwa mfano wa maadili mema,” amesisitiza Dkt. Jingu.

‎Katika ziara hiyo, Dkt. Jingu pia alitumia fursa hiyo kusikiliza baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi na uongozi wa chuo hicho, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la hosteli, ukarabati wa majengo chakavu pamoja na upungufu wa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo katika karakana ya Chuo.


‎Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi,  Emanuel Mhagama amesema ujio wa Katibu Mkuu ni faraja kubwa kwa Chuo hicho na umeongeza hamasa kwa wanafunzi na walimu huku akisema Chuo kimejipanga kuhakikisha kinatoa wahitimu wenye ujuzi na maadili bora ambao wataweza kuchangia maendeleo ya jamii zao. 

‎Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii,  Juliana Kibonde amesema amefarijika kuona idadi kubwa ya wasichana chuoni hapo wakisoma masomo ya sayansi na ufundi, jambo linaloonesha mabadiliko chanya katika jamii na ni fahari kuona wasichana wanasoma masomo ambayo zamani yalihesabiwa kuwa ni ya wavulana  pekee.


Katika ziara hiyo, Dkt. Jingu pia alitumia fursa hiyo kusikiliza baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi na uongozi wa chuo hicho, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la hosteli, ukarabati wa majengo chakavu pamoja na upungufu wa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo katika karakana ya Chuo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi,  Emanuel Mhagama amesema ujio wa Katibu Mkuu ni faraja kubwa kwa Chuo hicho na umeongeza hamasa kwa wanafunzi na walimu huku akisema Chuo kimejipanga kuhakikisha kinatoa wahitimu wenye ujuzi na maadili bora ambao wataweza kuchangia maendeleo ya jamii zao. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii,  Juliana Kibonde amesema amefarijika kuona idadi kubwa ya wasichana chuoni hapo wakisoma masomo ya sayansi na ufundi, jambo linaloonesha mabadiliko chanya katika jamii na ni fahari kuona wasichana wanasoma masomo ambayo zamani yalihesabiwa kuwa ni ya wavulana  pekee.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO