JAMII IELIMISHWE KUWALINDA WATOTO MITANDAONI- WAKILI MPANJU


Na WMJJWM-Dodoma.

Serikali inaendelea  na juhudi kuhakikisha  inawalinda Watoto  dhidi ya maudhui yanayoweza kuwapotezea dira na muelekeo  wa maisha mtandaoni ili kuweza kujenga taifa lenye maadili na watu wanaojitambua.

Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju katika kikao kazi cha kamati ya Taifa ya ushauri juu ya usalama na ulinzi wa watoto mitandaoni kilichofanyika Julai 09,2025 Jijini Dodoma.

Wakili Mpanju amefafanua kwamba elimu ya kuwalinda watoto mtandaoni ni muhimu  kutolewa  kwa jamii hususan kwa wazazi, walezi  na walimu ilikupata uelewa  na wao waweze kuwekeza  juhudi  katika vita ya kumlinda mtoto dhidi ya madhara anayoweza kupata mtoto anapotumia vifaa vya kielektroniki ipasavyo.

“Ni lazima  tuielimishe jamii juu ya mabadiliko ya teknolojia  kupitia majukwaa sahihi  ili kuwalinda watoto kwani wao ndiyo wanaokaa nao muda mwingi  lakini vilevile  utekelezaji wa sheria bila kuwa na elimu juu ya masuala haya tutakuwa hatujatimiza wajibu wetu “amesema Mpanju.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa  idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka wizara ya Maendeleo ya Jami,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema kikao kazi hicho kimedhamiria kukamilisha mpango kazi wa Taifa juu ya matumizi ya laini za simu za watoto ili  mamlaka husika ziweze kufuatilia mienendo ya watoto na kuwa rahisi kutambua pale ambapo watoto wanapokua hatarini.

Naye mkurugenzi msaidizi  kutoka Ofisi ya Rais- Tamisemi Subisya Kabuje  amesema   ofisi ya Rais-Tamisemi itashirikiana na Wizara ya Maendeleo yq Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kuhakikisha watoto wanakuwa salama kupitia  Kuratibu  utekelezaji wa afua za kumlinda mtoto mtandaoni katika tawala za Mikoa na  Serikali za mitaa  kwa kuhakikisha mifumo inasomana na kurahisisha  zoezi hilo.






 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO