Posts

Showing posts from July, 2026

*CHANDA CHEMA HUVIKWA PETE*

Image
Maafisa na askari  wa jeshi la Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro waliopoteza maisha, kujeruhiwa na kufanya kazi kwa uhodari wametunukiwa vyeti na fedha kutokana na kujitoa kwao kwa hali na mali kulinda rasilimali za wanyamapori na misitu. Tuzo hizo zimetolewa tarehe 31 Julai 2026 kwenye maadhimisho ya  siku ya  askari wanyamapori duniani ambayo huadhimishwa kwa lengo la kuutambua mchango wa  askari hao katika kulinda rasilimali za nchi na kuenzi mchango wa Askari 10 waliopoteza maisha yao na kujeruhiwa wakiwa kazini katika hifadhi ya Ngorongoro. Naibu kamishna wa Uhifadhi huduma za shirika Aidan Makala  amewapongeza askari wote wa jeshi la uhifadhi kutokana na  kujitoa kwa hali na mali katika kazi hiyo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kulinda matakwa ya haki jinai. Naibu Kamishna Makala ameleza kuwa,  askari  wa  uhifadhi ni nguzo ya ulinzi wa rasilimali za wanyamapori  na misitu ambapo...

MD TWANGE AWATAKA WANASHERIA WA TANESCO KUENDELEA KUSIMAMIA MAADILI NA TAALUMA*

Image
📌 Afungua Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO jijini Mwanza 📌 Awasisitiza kutoa ushauri wa kisheria kwa wakati na kulinda maslahi ya Shirika Na Mwandishi Wetu, Mwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, amewataka wanasheria wa shirika kuendelea kusimamia maadili ya taaluma, kutoa ushauri wa kisheria kwa wakati na kulinda maslahi ya shirika ili kuimarisha utendaji na kuhakikisha TANESCO inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Bw. Twange ameyasema hayo wakati akifungua Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO lililoanza Julai 28, 2026 jijini Mwanza, likiwakutanisha wanasheria kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda na Kampuni Tanzu za TANESCO kwa lengo la kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kisheria yanayohusu utendaji wa shirika. Akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo, Bw. Twange amewapongeza wanasheria hao kwa mchango wao katika kulinda maslahi ya shirika na kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia sheria na tar...

*WHERE HUMANITY BEGINS, WONDER ENDURES*

Image
Some places are admired for their beauty. Others are remembered for the stories they hold. Ngorongoro is both. Addressing the 48th Session of the UNESCO World Heritage Committee in Busan, Republic of Korea, the Ngorongoro Conservation Area Authority Conservation Commissioner Abdul-Razaq Badru reminded the world that humanity, like a river, has a source. "A river that forgets its source will one day run dry," he reflected, calling on us to honour our beginnings if we are to shape a stronger future. In Ngorongoro, the story of humanity is not confined to museums or history books; it lives in the landscapes, the fossils, the footprints and the enduring connection between people and nature. His message reached far beyond conservation. It was a reminder that understanding where we come from gives us the wisdom to decide where we are going. Ngorongoro is more than a remarkable destination; it is a place where our shared human journey continues to speak across generations. Every pre...

*MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA MSONGO WA KILOVOLTI 400 CHALINZE–DODOMA MBIONI KUKAMILIKA*

Image
📌 Wafika asilimia 94 ya utekelezaji wake 📌 Kazi za uvutaji waya kwenye mradi kusababisha katizo la muda la umeme katika baadhi ya maeneo kwa ratiba maalumu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma uko kwenye hatua za mwisho za utekelezaji wake, huku ujenzi ukiwa umekamilika kwa asilimia 94 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 21, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 28, 2026, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, amesema ili kuwezesha ukamilishaji wa kazi za mradi huo kutakuwepo na katizo la muda la umeme katika baadhi ya maeneo nchini kwa ratiba maalumu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakua Julai 30 hadi Agosti 4 na ya pili itaanza Agosti 11 hadi 17, 2026. Gowelle amesema hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya ombi la Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kampuni ya TBEA ambayo inalenga kuhakikisha kazi zinafanyika kwa hali...

MTENDAJI MKUU WA TARURA MHANDISI VICTOR SEFF AMKABIDHI ZAWADI YA KITABU BI CATHERINE SUNGURA

Image
Dodoma Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amekabidhiwa zawadi ya kitabu kiitwacho ‘The Game of the Impossible’ na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Bi. Catherine Sungura. Kitabu hicho, kilichoandikwa na PEMANDU Associates ya Malaysia, kinaelezea uzoefu wa taasisi hiyo katika kuiwezesha Malaysia kutekeleza mageuzi makubwa ya kitaifa kupitia mifumo madhubuti ya utekelezaji wa sera, mipango na usimamizi wa matokeo.  Kitabu hicho kinatarajiwa kuwa rejea muhimu wakati TARURA inaenda kutekeleza Mpango Mkakati wake wa tatu wa mwaka 2026/2027-2030/2031.

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU*

Image
Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini. 📌Mradi utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 100   📌Aeleza mradi kugharimu Shilingi bilioni 204.4 na kuchochea sekta za kilimo, viwanda na uchimbaji wa madini.   📌Aitaka TANESCO kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi ili ukamilike kwa wakati.   Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeingia hatua mpya ya kuongeza vyanzo vya uzalishaji umeme baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa umeme kwa nguvu ya Jua Kishapu utakaozalisha jumla ya megawati 100.   Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 50 na kuingizwa katika Gridi ya Taifa, jambo lililoongeza uwezo na uthabiti wa gridi hiyo na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.   Akizungumza katika hafla hiyo Julai 27, 2026, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema sekta ya nis...

DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Image
DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA Na Mwandishi Wetu.  Tafadhali Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa Dar Es Salaam, Tanzania.  Kufuatia kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini unaofanywa na Wizara ya Madini kupitia Kikosi Kazi (Taskforce), madini aina ya dhahabu Gramu 4,402.20 yenye thamani ya 1,238,458,594.42 yamekatwa yakitoroshwa. Hayo yamesemwa leo tarehe 27 Julai, 2026 na Waziri wa Madini,  Anthony Mavunde (Mb) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. "Serikali kupitia Wizara ya Madini iliunda Kikosi kazi ambacho kinahusisha vyombo vya dola ili kudhibiti biashara haramu ya madini na utoroshaji. Hii ni sehemu tu ya kazi ambazo zimeendelea kufanywa na Kikosi kazi hicho katika kuimarisha mfumo wa ufanyaji biashara ya madini" "Ndugu zangu, dhahabu hii yenye zaidi ya thamani ya bilioni 1.2 haikupitia katika mfumo rasmi wa ufanyaji biashara ya madini na hivyo kupelekea Serikali kukosa mapat...

WAKALA WA VIPIMO WASHIRIKI NBC MARATHON DODOMA*

Image
Watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) asubuhi ya leo Julai 26, 2026 wameshiriki katika mbio za *NBC Marathon* zilizozofanyika jijini Dodoma kwa uratibu wa *Benki ya NBC*. Lengo kuu la mbio hizo ilikuwa kukusanya fedha za kusaidia matibabu kwa wagonjwa wasiojiweza, pamoja na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa mazoezi katika kuimarisha afya. WMA imeshiriki katika mbio hizo kuunga mkono dhamira hiyo ya kibinadamu na kuonyesha mchango wa taasisi za Serikali katika masuala ya afya na ustawi wa jamii. Katika ushiriki huo, *watumishi 6 wa WMA walikimbia umbali wa Kilometa 10* wakati *mtumishi 1 alikimbia Kilometa 21*. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, *Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba* amewapongeza washiriki na waandaaji wa mbio hizo. Aidha ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kwa wingi katika matukio kama haya ili kufanikisha malengo ya kuwasaidia wagonjwa na kuimarisha afya ya Taifa. Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa WMA, Meneja wa Mkoa wa Dodoma, Ibrahim Saidi amesema, "Tume...

_MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI, AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA OACPS*

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki, mazungumzo yaliyofanyika Jijini Arusha.   Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amemuhakikishia Katibu Mkuu wa OACPS dhamira ya Tanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kuleta mageuzi na kuifanya kuwa na tija kwa nchi wanachama.   Aidha amempongeza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OACPS kwa kutekeleza ajenda ya mageuzi ikiwa ni pamoja na kuongeza uadilifu na kupunguza utegemezi kwa lengo la kufanya Taasisi hiyo kuwa na nguvu zaidi.   Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki ameeleza kuhusu vipaumbele vya Taasisi hiyo ikiwemo suala la kuimarisha biashara, kuimarisha mtangamano miongoni mwa nchi wanachama, kujenga uhimilivu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia...

*KARIBU NYUMBANI, NGORONGORO IMEWAFIKIA OMAN*

Image
  Mwambata wa ubalozi  wa Oman nchini Tanzania, Abdulrahman Salim Algaad akiwa na familia yake, ametembelea Hifadhi ya Ngorongoro  na kushuhudia maajabu ya utalii yaliyopo katika kivutio namba moja cha utalii barani afrika   Akimpokea mwambata huyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko  Mariam  Kobelo ameeleza kuwa jitihada za mamlaka hiyo kuwafikia wadau mbalimbali zimeendelea kuzaa matunda ambapo watumishi kutoka balozi mbalimbali ndani na nje ya nchi wamendelea kutembelea hifadhi hiyo.   Akiwa ndani ya hifadhi hiyo, Abdulrahman Algaad na familia yake walipata fursa ya kushuhudia wanyamapori adimu wakiwa katika mazingira yao ya asili, wanyamapori wakubwa watano, misitu, maporomoko ya maji, urithi wa utamaduni na mambo kale, makumbusho ya urithi geopark na kueleza kuwa ndoto na hisia alizokuwa nazo zimekutana na uhalisia.   Mwambata huyo ameonyesha kuvutiwa na uzuri wa Hifadhi ya Ngorongoro na vivutio v...

MAAFISA RASILIMALI WATU TANESCO WAPONGEZWA KWA UTULIVU MAHALA PA KAZI.

Image
📌 Ni katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌Wasisitizwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi  

FROM NAINOKANOKA TO MSOMERA: A NEW CHAPTER OF HOPE*

Image
For the Saitoti family, the relocation from Nainokanoka ward in Ngorongoro conservation area to Msomera Handeni Tanga represented far more than a geographical transition; it marked the commencement of a new chapter of new better future. That chapter is now distinguished by profound joy. On July 18, 2026, Evaline Saitoti, a young Maasai woman who resettled in Msomera with her family, solemnized her marriage and was welcomed into an American family currently residing in Zanzibar. The union constitutes not only a significant personal milestone but also exemplifies the emerging opportunities that have followed the family's voluntary relocation. “Unlike Ngorongoro, Our life in Msomera has been characterized by opportunity, good life status surrounded by social services like schools, health centers, electricity, street road network, communication facilities and practice our traditional culture peacefully and safe” stated her elder brother, Emmanuel Saitoti.  “We have established a new ho...

*WAZIRI MAVUNDE AANZA ZIARA RASMI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI MKOANI GEITA**

Image
*▪️ Waziri Mavunde ni Mlezi wa shughuli za kimaendeleo mkoani Geita* *▪️ Akagua mradi wa maji wa Bilioni 40 ambao utanufaisha watu 185,000* *▪️ Akagua mradi wa vijana wa ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua madini* *▪️ Aweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Rwantaba* *Chato, Geita** Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameanza ziara rasmi ya kikazi mkoani Geita kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuhamasisha shughuli za kiuchumi na kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayolenga kuboresha maisha ya wananchi. Mhe. Mavunde, ambaye pia ni Mlezi wa shughuli za maendeleo mkoani Geita, anatarajiwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika halmashauri na wilaya za mkoa huo, sambamba na kuzungumza na wananchi kuhusu fursa za maendeleo na mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa Taifa. Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri Mavunde amekagua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 40, unaotaraj...