*KAIMU MENEJA MKUU TGDC ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA*




Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mha. Shakiru Idrissa Kajugus, ametembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mha. Kajugus amepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Nishati  kwa wananchi wanaotembelea banda hilo.

Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, ikiwemo umeme, gesi asilia, nishati safi ya kupikia na maendeleo ya miradi ya kimkakati, katika banda lake lililo karibu na banda la TANESCO.


Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO