*MHA. MRAMBA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA*




Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambayo leo yanafikia kilele katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Wizara, Mhandisi Mramba amepata maelezo kutoka kwa wataalam wa Wizara ya Nishati kuhusu elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo. 

Elimu hiyo inahusu  huduma zinazotolewa na Wizara na Taasisi zake pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya nishati, ikiwemo umeme, mafuta, gesi asilia, nishati jadidifu na nishati safi ya kupikia, sambamba na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati nchini.



Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO