MKURUGEZI WA KITENGO CHA UKUZAJI TIJA KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU YOHANA MADADI ATEMBELEA BANDA LA TARURA



Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukuzaji Tija kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano Kazini) Bw. Yohana Madadi ametembelea banda la pamoja la Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake ambapo Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa TARURA Bi. Catherine Sungura amempa maelezo kuhusu majukumu ya TARURA hususani Mpango wa CBRM.

Bi Sungura amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Mpango wa CBRM kwa kutumia vikundi vya kijamii utachochea ongezeko la tija kwa wananchi wa maeneo husika kwa kuwapatia fursa za ajira na kipato. 

Aidha, ameeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utasaidia kuhakikisha barabara nyingi nchini zinapitika wakati wote hivyo kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi nchini.

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO