*CHUMA CHIKOLI MOTO NGORONGORO




Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Mariam Chuma Kobelo, ametunukiwa tuzo ya _Iconic Woman in Tourism Promotion_ katika hafla ya Ladies Talk Awards & Dinner 2026 iliyofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Morogoro.

Bi Mariam ametwaa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza na kutangaza utalii wa Tanzania kupitia ubunifu wa kampeni za masoko, usimamizi wa huduma za utalii, pamoja na juhudi za kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa kupitia eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Kupitia uongozi wake, Ngorongoro imeendelea kujijengea sifa kama moja ya vivutio vya utalii wa kifahari (Premium destination) vinavyoongoza barani Afrika, na kusimamia utekelezaji wa kampeni mbalimbali za masoko zinazolenga kuongeza idadi ya watalii na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika maendeleo ya utalii endelevu.

Utambuzi huo unaongeza rekodi ya mafanikio ya kamishna Kobelo, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta  masoko mapya ya utalii wa Ngorongoro ndani na nje ya nchi, pamoja na kuratibu programu zinazochangia ukuaji wa sekta ya utalii na kuimarisha juhudi za uhifadhi.

Kamishna Mariam Kobelo ameishukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro chini ya usimamizi wa kamishna wa uhifadhi wa mamlaka  hiyo Abdul-Razaq Badru kutokana na ushirikiano mkubwa katika kukuza vipaji vya watumishi na kuviendeleza.




Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO