Posts

Showing posts from August, 2026

RAIS SAMIA AZINDUA RASMI KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA BWAWA LA JULIUS NYERERE.*

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 leo, tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, mkoani Pwani. Viongozi mbalimbali wameungana na Rais Samia katika uzinduzi huo, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Moustafa Madbouly; Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi; pamoja na viongozi wengine. Uzinduzi wa JNHPP ni kilele cha utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati uliotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huo umegharimu takribani shilingi trilioni 7.452, sawa na dola za Marekani bilioni 3.35. Ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025. JNHPP imeongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini na kuimarisha usalama wa nishati. Kwa sasa, u...

RAIS SAMIA AWASILI JNHPP

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi na viongozi wengine wakati alipowasili katika eneo la Mradi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP). Rais Samia atazindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 leo tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA ENEO LA HAFLA YA UZINDUZI WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (JNHPP)

Image
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kumiminika katika eneo la hafla ya uzinduzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), wakishuhudia tukio hilo muhimu katika historia ya maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Hafla hiyo inafanyika leo, huku wananchi na wageni mbalimbali wakifika katika eneo la tukio kushiriki katika tukio hilo kubwa linalohusisha uzinduzi rasmi wa mradi huo wa kimkakati wa kuzalisha umeme. Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuzindua rasmi Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuzungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali watakaoshiriki katika hafla hiyo.

WAZIRI KOMBO APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KWA BALOZI MTEULE WA UBELGIJI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati  za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ubelgiji nchini Mhe. Lot Debruyne, katika Ofisi ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam.  Baada ya tukio hilo viongozi hao walijadili namna bora ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji. Akizungumza na Balozi Mteule wa Ubelgiji Mhe. Waziri Kombo alisisitiza azma ya kuhamisha ushirikiano kutoka kwenye misaada na kuelekea katika kufanya biashara na uwekezaji. Mhe. Waziri Kombo ameeleza juu ya fursa za ushirikiano katika kilimo na umwagiliaji, uhamishaji wa maarifa na ujuzi, pamoja na mitambo na teknolojia za kisasa za kilimo.  Pia alihimiza kuongezwa kwa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji akitaja ongezeko la watalii kupitia safari za moja kwa moja za Shirika la Ndele la Ubelgiji (Brussels Airlines) kwenda Kilimanjaro na Zanzibar kama fursa ya...

PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

Image
Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari na maelekezo yanayotolewa na wataalamu na mamlaka husika ili kupunguza madhara yanayotokana na majanga na maafa. Prof. Kabudi ametoa wito huo tarehe 19 Agosti, 2026 wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. “Ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga, huku akiwataka kuendelea kufuata taarifa na maelekezo rasmi kutoka kwa wataalamu na mamlaka zinazohusika na masuala ya maafa.” Katika hatua nyingine, alisema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema na kujenga ustahimilivu wa jamii ili kuongeza uwezo wa wananchi kukabiliana na majanga na kupunguza madhara yanayotokana na matukio hayo. Alisema uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga kwa ufanisi unategemea uwepo wa mifumo madhubuti,...

Serikali yasisitiza ushirikiano na Sekta Binafsi ( PPP)

Image
Serikali yasisitiza ushirikiano na Sekta Binafsi ( PPP) Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuongeza uwekezaji na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Maji katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2024 hadi 2025. Waziri Aweso amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi, sambamba na kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za maji nchini. Amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji vijijini, kwasababu Serikali inalenga kumaliza uhaba wa maji katika vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya huduma ya maji. Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuzielekeza ka...

ZAIDI YA WATU 20 WAHOJIWA SAME KWA TUHUMA ZA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI

Image
ZAIDI YA WATU 20 WAHOJIWA SAME KWA TUHUMA ZA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI Na Musa Mathias,  Same, Kilimanjaro.  Tafadhali Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa Zaidi ya watu 20 wanahojiwa na Jeshi la Polisi wilayani Same kwa tuhuma za kudaiwa kuendesha shughuli za uchimbaji haramu wa madini katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kinyume cha sheria na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira. Akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amesema Kamati ya Usalama ya wilaya ilipata taarifa za siri kuhusu uchimbaji huo katika maeneo mbalimbali na kufika kujiridhisha, ambapo ilibaini kuwepo kwa shughuli hizo. Amesema baada ya kubaini hali hiyo, Kamati iliunda timu ya kwanza ya wataalamu kutoka RUWASA, Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Maafisa Mazingira na Maafisa Madini, iliyofanya uchunguzi katika maeneo yote na kubaini uchimbaji haramu katika kata saba pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira. Aidha, iliundwa timu ya pili kutoka ndani ya Kama...

VIKUNDI VYA CBRM VYATAKIWA KUWA WALINZI WA BARABARA ITILIMA

Image
‎ ‎Itilima, Simiyu ‎ ‎Vikundi vya kijamii vinavyotekeleza matengenezo ya kawaida ya barabara kupitia Mpango wa CBRM unaotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) vimetakiwa kushirikiana na wananchi katika kulinda na kutunza miundombinu ya barabara ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii. ‎ ‎Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Anna Gidarya wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha jumla ya vikundi 16 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi shughuli za matengenezo madogo madogo ya barabara katika maeneo yao. ‎ ‎Mhe. Gidarya amesema barabara ni mali ya wananchi na ni sehemu muhimu ya kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo amewataka wanavikundi pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kuzilinda dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu hiyo. ‎ ‎Aidha, amevipongeza vikundi hivyo kwa kupata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika matengenezo ya barabara akieleza kuwa hatua hiyo si tu inasa...

CHEREKO CHEREKO BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO.*

Image
Kamati tendaji ya Baraza la Wafugaji  tarafa ya Ngorongoro imekutana leo tarehe 18 Agosti, 2026 ambapo pamoja na mambo mengine imechambua na kupitisha orodha ya majina ya wanafunzi wa kidato cha tano kutoka kata 11 za tarafa ya Ngorongoro wanaofadhiliwa na Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro Majina ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Ngorongoro yanatokana na mapendekezo ya  kata zote 11 zenye Vijiji 25 ambapo kila kata inachagua wanafunzi watatu (03) ambapo wanapata fursa hiyo ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha uhusiano kati ya Ngorongoro na Jamii inayoishi ndani ya hifadhi Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa sambamba na kusaidia huduma  za elimu kwa wanafunzi wa tarafa ya Ngorongoro, katika kipindi cha wiki moja ijayo itafanyika tathmini ya mahitaji ya maji na barabara zenye changamoto ambapo Ngorongoro inatarajia kuchimba visima  saba  (07) na kukarabati mtandao wa barabara katika maeneo ya hifadhi ili kuhudumia wananchi na watal...

MKAKATI WA TAIFA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA WAANZA KUTEKELEZWA MKINGA*

Image
πŸ“Œ*Mitungi ya gesi ya kilo sita 3,255 kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 17,500* πŸ“*Mkinga, Tanga* Serikali imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga, kupitia mradi wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku. Kupitia mradi huo, jumla ya mitungi 3,255 ya gesi ya kilo sita itasambazwa na kuuzwa kwa wananchi wa Mkinga kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 17,500 kwa mtungi. Mwananchi anayehitaji kunufaika na mpango huo anatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Mtungi huo utauzwa ukiwa tayari kwa matumizi, ukiwa na gesi pamoja na vifaa muhimu. Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, unaolenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. Utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya nishati safi, salama na rafiki kwa afya na mazingira, huku ukipun...

NI DHAMBI KUBWA KWA MWANAUME WA KIHADZABE KUTAHIRIWA.

Image
Wahadzabe ni kabila linalopatikana mkabala na ziwa Eyasi pembezoni mwa hifadhi ya Ngorongoro na habari za maisha yao zimehifadhiwa katika makumbusho ya Urithi Jiopaki liyopo Karatu Mkoani Arusha. Pamoja na mabadiliko ya ulimwengu na elimu kutolewa lakini kabila hili bado haliamini katika tohara kwa kijana wa kiume, kwao hiyo ni mwiko wakiamini binadamu anastahili kuwa kama alivyozaliwa. Sababu kubwa ya kutokutahiriwa ni kuwa ukitahiriwa unapunguza nyama ya binadamu na kuizika wakati binadamu huyo akiwa hai, imani ni kwamba huwezi kata sehemu yoyote ya mwili wa binadamu aliye hai Vilevile kabila  hili linaamini kwamba mwanaume akitahiriwa hupunguza ukubwa na utaalam wa mambo na kufanya  mwili wako kuwa na mapungufu hata wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Katika kuhakikisha kwamba mwanaume anakuwa na nguvu za kutosha wakati wa kushiriki tendo la ndoa hulazimika kula mizizi inayopatikana porini , matunda, asali ikiwa fresh na nyama pori ambayo inachomwa au kuchemshwa supu. Kutoka...

*DKT.SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22*

Image
πŸ“Œ*Waziri Ndejembi asema  ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni*  πŸ“Œ*Asema mradi wa JNHPP ni matokeo ya uwekezaji wa sh.trilioni 7.4; Fedha za Watanzania* Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani. Amesema hayo tarehe 15 Agosti, 2026 jijini Dar es Salaam  katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo utakaohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wageni kutoka ndani na nje ya nchi, wananchi na wadau wa maendeleo. " Uzinduzi huu wa mradi wa umeme wa  Julius Nyerere ni tukio la kihistoria na hatua muhimu katika safari ya Tanzania ya kujenga mfumo wa nishati ya uhakika nchini, sambamba na kuchochea shugh...

*SEKTA YA MADINI YAVUTIA UWEKEZAJI WA TRILIONI 9 NDANI YA MIAKA MINNE*

Image
▪️Mikataba ya Msingi 14 ya Madini Yasainiwa ▪️Serikali yasaini Mkataba wa Bilioni 265 na Kampuni ya Henan Yudi Mining ya Mradi wa Graphite Morogoro ▪️Tanzania yawa kivutio kikubwa cha uwekezaji sekta ya Madini Afrika ▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji πŸ“MOROGORO:  Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema ndani ya kipindi cha Miaka Minne, (4)  Sekta ya Madini imevutia uwekezaji wa Shilingi trilioni 9, hatua inayoiweka Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji wa Madini Barani Afrika. Amesema hayo leoAgosti 15, 2026, Mkoani Morogoro wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari jumla ya mikataba ya Msingi 14 imekwisha sainiwa. Amesema kuwa mradi huo una mashapo yaliyothibitishwa ya takribani tani milioni 104.28 za kinywe, na unatarajiwa kuwekeza takribani Dola milioni 100 (Shilingi bilioni 265) huku uzalishaji wa kiwango kamili ukile...