Posts

Showing posts from May, 2025

MASHINDANO YA UMITASHUNTA KUFANYIKA MKOANI IRINGA KITAIFA

Image
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA na yale ya Shule za Sekondari UMISSETA kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kuanzia Juni 7,2025. Mashindano hayo yatajumuisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, yakihusisha michezo mbalimbali kama soka kwa wavulana na Wasichana,Mpira wa kikapu, Netiboli,Wavu na Riadha. Michezo mingine ni mpira wa Goli ambao ni maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye uono hafifu, pamoja na Sanaa za Michezo na Burudani ambayo inahusisha ngoma za asili, kwaya na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor). Mashindano hayo pia yatajumuisha michezo mingine kwa wanafunzi wenye ulemavu, ikiwepo soka Wasichana na Wavulana pamoja na Riadha. UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 inaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.

RUAHA YAFANYA KIKAO NA WADAU WA UTALII KUELEKEA MSIMU MPYA WA UTALII - IRINGA.*

Image
Na. Jacob Kasiri - Iringa. Katika kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa utalii (high season) Juni, 2025, Hifadhi ya Taifa Ruaha imeendesha kikao maalumu kilichowakutanisha wadau wa utalii ili kujadili  Masuala mbalimbali kuhusu shughuli za Utalii,changamoto na mikakati ili kukuza utalii ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.  Kikao hicho cha siku moja kilichofanyika jana Mei 30, 2025 katika Ukumbi wa Sunset Hotel mjini Iringa kimewajumuisha TANAPA, Mawakala wa Utalii, waongoza watalii (Guides), Mawakala wa Usafirishaji, wamiliki wa hoteli, wawakilishi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wizara ya Maliasili na Utalii-Kusini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Uhamiaji na Polisi. Akielezea umuhimu wa kikao hicho Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Abel Mtui alisema,  “Wadau wote waliojumuika katika kikao hicho ni muhimu katika mnyororo mzima wa utalii ili kufikia maazimio ya pamoja katika kukuza sekta ya utalii Nyanda za juu Kusini na Tanzania kwa ujumla. Aid...

WARATIBU WATAKIWA KUIMARISHA URATIBU NA UTEKEZAJI WA MTAKUWWA

Image
Na WMJJWM - Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju ametoa wito kwa Waratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kuhakikisha wanaimarisha uratibu na utekelezaji wa mpango huo katika ngazi za mikoa na halmashauri. Akizungumza katika kikao kazi cha waratibu wa MTAKUWWA kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara kilicholenga kuwapatia Mafunzo kuhusu uratibu na utekelezaji wa Mpango Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma kinalichoanza  Mei 28 hadi 31 , 2025, Mpanju amesema kikao hicho ni muhimu katika kujenga uelewa kuhusu uratibu wa MTAKUWWA II (2024/25 – 2028/29)  Wakili Mpanju amesema Waratibu wa MTAKUWWA ni kiungo muhimu katika kuhakikisha afua za mpango huo zinatekelezwa kikamilifu na ni lazima wasimame imara, washirikiane na maafisa wa mikoa, halmashauri na wadau wote ili kua...

VIJANA 26 KUSHIRIKI PROGRAMS YA MANDELA WASHINGTON FELLOWSHIP 2025 NCHINI MAREKANI

Image
Vijana waliochaguliwa kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship kwa mwaka 2025, wamekumbushwa kuwa fursa waliyoipata haikuja kwa bahati, isipokuwa kutokana na majukumu wanayoyafanya ambayo yana mchango mkubwa kwa jamii. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa wakati anawapa nasaha za kuwaaga vijana hao 26 jijini Dodoma Mei 30, 2025. Balozi Mussa aliwataka kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mapya kwa kuwa nchi wanayokwenda imeendelea kiuchumi na kiteknolojia duniani na itawapa fursa pia ya kukutana na raia wa mataifa mbalimbali wenye uzoefu na mila tofauti. Vijana hao ambao wanatarajiwa kwenda nchini Marekani Juni na kurejea Agosti 2025,  wametakiwa kulitangaza jina la Tanzania kwa watu watakaokutana nao. "Mtalitangaza jina la nchi yetu kwa kuheshimu sheria za nchi mnayokwenda,  kutangaza utamaduni mzuri wa Tanzania na kuelezea kwa ufasaha mambo makubwa na mazuri ya nchi kama vile mlima K...

MIRADI 12 TANGA YABAINIKA KUWA NA MAPUNGUFU KATI YA MIRADI 54 YA MAENDELEO TAKUKURU YABAINI.

Image
Na,Agnes Mambo,Tanga. TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru)imefanikiwa kufuatilia miradi ya maendeleo 54 yenye thamani ya shilingi Billion 240,264,703,118 Kwa kipindi Cha mwezi January hadi machi na kubaini mapungufu miradi 12 yenye thamani ya shilingi Billion 5,468,760,058  Akizungumza na wanahabari Mkoani Tanga Mei 30/2025 Kaimu mkuu wa Tangukuru mkoa wa Tanga Mariamu Mayaya Kwanimba ya Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah. Amesema katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo walibaini miradi yenye mapungufu  12 na kuitolea ushauri wa marekebisho. Miradi hiyo iliyokuwa na mapungufu ilikuwa ya sekta ya Afya,Elimu,na Sekta ya Maji. Kamanda Mayaya amesema katika ufuatiliaji wa kina kwenye miradi hiyo ya maendeleo 54 ambapo miradi 12 ilibainika kuwa na mapungufu ambapo ushuri wa marekebisho ulitolewa na hatua za marekebisho ya mapungufu hayo zimechukuliwa. "Hivi sasa miradi hiyo Ipo katika Hali inayokidhi ubora kulingana na thamani ya fedha zi...

WAKULIMA WA PARACHICHI WAPONGEZA RUZUKU YA MBOLEA, WAPENDEKEZA UTAFITI MBOLEA MAHALUM YA PARACHICHI*

Image
Wakulima wa parachichi mkoani Njombe wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia mbolea ya ruzuku ambayo imewasaidia kuongeza tija na uzalishaji katika zao hilo. Wakizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) walipotembelea Chama cha Msingi cha Ng’anda AMCOS na kampuni ya mkulima wa parachichi ya Avo Nemes Green Limited, tarehe 28 Mei, 2025, wakulima hao walisema ruzuku hiyo imepunguza gharama za uzalishaji na kuwawezesha kuajiri nguvu kazi zaidi kwenye mashamba yao. Mkulima mkubwa wa parachichi, Bw. Stephen Mlimbila, alieleza kuwa kupitia ruzuku hiyo, amepunguza gharama na fedha alizokuwa akizitumia kununua mbolea sasa zimeelekezwa kwenye ulipaji wa vibarua wanaohudumia shamba lake lenye ukubwa wa ekari 210 na kuwa chanzo cha ajira kwa wananchi wengi wasiokuwa na kazi. Akijibu ombi la wakulima wa chama cha Ushirika Ng’anda cha kusajiliwa kuwa wakala wa mbolea za ruzuku, Kaimu M...

SERIKALI NA WADAU WATATHIMINI UIMARISHWAJI USAWA WA KIJINSIA

Image
Na WMJJWM-Dodoma Serikali imeendesha kikao cha tatu cha Kamati Tendaji ya Mpango wa Taifa wa Usawa wa Kijinsia, kilicholenga kutathmini mafanikio, changamoto na hatua zilizochukuliwa katika kuimarisha usawa wa kijinsia nchini. Kikao hicho, kimefanyika katika ukumbi wa Domiya Estate jijini Dodoma, kimewaleta pamoja washiriki zaidi ya 65 kutoka serikalini, sekta binafsi, Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali na wadau wa maendeleo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia (2021–2027) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU). Akizungumza kwenye kikao hicho Mei 29,2025 Jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, amesema kikao hicho kimechochea mijadala muhimu kuhusu sababu za kiwango cha chini cha utoaji taarifa za ukatili wa kijinsia pamoja na mikakati ya kuboresha huduma za madawati ya kijinsia shuleni na kwenye jamii. “Tunaendelea kufanya tathmini ya kina kuhusu namna wanawake wanavyoshiriki...

DKT. BITEKO ATAJA MAENEO SITA YA VIPAUMBELE UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2020/2025

Image
📌 CCM yajivunia kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii 📌 Rais Samia asema CCM kuzindua Ilani yake kesho 📌 CCM yazalisha ajira 800,000 kwa vijana 2020/2025 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita aliyowasilisha ni ya mwisho katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020.  Amesema hayo Mei 29, 2025 wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum wa  CCM Taifa - 2025 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.  Ametaja maeneo sita muhimu ya vipaumbele  katika utekelezaji wa Ilani hiyo ya CCM kuwa ni pamoja na kulinda  na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa. Dkt. Biteko ameendelea kwa kusema kuwa eneo lingine ni kukuza  uchumi w...

KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI*

Image
📌  Lengo ni kuhakikisha kila Jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na umeme* 📌 Vinahusisha mahitaji ya kiuchumi na Kijamii, ukubwa wa Jimbo na Kitongoji* *📌  Mkurugenzi Mkuu REA atakiwa kumsimamia kwa karibu Mkandarasi wa miradi ya Vitongoji Ziwa Tanganyika* Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza miradi ya umeme katika Vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada ikiwemo ukubwa wa vitongoji, ukubwa wa Jimbo pamoja na mahitaji ya kiuchumi na kijamii. Lengo la kuweka vigezo hivyo ni kuhakikisha kuwa kila jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na nishati ya umeme. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 29, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Olesendeka aliyeuliza kwamba  Serikali imejipangaje kutekeleza miradi ya Vitongoji kulingana na jiografia ya Wilaya ya Simanjiro ambapo umbali kutoka Kitongoji kimoja hadi kingine ni zaidi ya...

NCAA YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA UTALII KUHUSU MATUMIZI YA MFUMO MPYA WA SAFARI PORTAL V2.*

Image
Na Kassim Nyaki, NCAA . Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Mei, 2025 kwa wadau wa Utalii kuhusiana na matumizi ya mfumo mpya wa *Safari Portal V2* ulioboreshwa kutoka mfumo wa zamani wa Safari Portal. Akifungua Mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Huduma za Utalii na masoko NCAA, Afisa Uhifadhi Mkuu Peter Makutian ameeleza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wadau wote wa Utalii kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa makusanyo ya mapato yatokanayo na shughuli za Utalii ambao umeboreshwa ili kurahisisha utoaji huduma kwa wadau wote wanaofanya kazi na NCAA. "Tumeboresha mfumo wetu wa makusanyo ya mapato ya Utalii na utaaanza kutumika kuanzia tarehe  31/05/2025, kwa hiyo ni muhimu wadau wetu wanaopata huduma kupitia mfumo huu wawe na uelewa ya maboresho yaliyofanyika na kuwasaidia namna ya kuhamisha taarifa zao kwenye mfumo mpya kabla ya tarehe ya kuanza mfumo huo" alilisitiza Makuatian. Makutian ameongeza kuwa sababu zilizo...

DCEA YATOA MAFUNZO WILAYANI SAME KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Image
DCEA YATOA MAFUNZO WILAYANI SAME KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA. Same, Kilimanjaro .  Katika harakati za kitaifa za kuikomboa jamii dhidi ya janga la dawa za kulevya, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, imeendesha mafunzo maalum kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi vitongoji wilayani Same, mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo, yameyofanyika leo Mei 29, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ambayo yamelenga kuwawezesha viongozi hao kutambua, kuzuia na kushughulikia changamoto zinazotokana na matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya, huku yakisisitiza maadili, uwajibikaji na ushirikiano wa kijamii katika mapambano hayo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mheshimiwa Kasilda Mgeni, amesema kuwa dawa za kulevya si tu kwamba zina madhara ya kiafya kwa binadamu, bali pia zinachangia kudhoofisha uchumi, kuvuruga familia, kusababisha kuporomoka kwa maadili, kupunguza nguvu kazi ya...

SAME KAYA SACCOS YARUDISHA FADHIRA KWA JAMII KWA KUTOA MSAADA WA VIFAA NA MAITAJI MUHIMU

Image
Na Ashrack Miraji kipeo Online Media  Katika kuendeleza uwajibikaji kwa jamii, taasisi ya kifedha ya SAME KAYA SACCOS imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa makundi yenye uhitaji katika Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro. Msaada huo umetolewa kama sehemu ya kuadhimisha mchango wa jamii katika mafanikio ya SACCOS hiyo, ikiwa ni mfano bora wa taasisi za kifedha kurudisha kwa jamii wanakotoka. Kwa mujibu wa Meneja wa SAME KAYA SACCOS, Bi Elvera Mdee, taasisi hiyo imetumia jumla ya Shilingi milioni tano (Tsh. Mil 5) katika kugharamia ununuzi wa bidhaa hizo, ambazo ni pamoja na vyakula, vinywaji, sare za shule (uniforms), vifaa vya usafi na vifaa vya shule (stationery). Walengwa wa msaada huo ni pamoja na hospitali ya Wilaya ya Same, Shule ya Sekondari Chauka iliyopo Hedaru, pamoja na kituo cha kulelea yatima cha Rafiki Children Centre kilichopo mjini Same. Kila taasisi ilipokea msaada kulingana na mahitaji maalum yaliyobainishwa awali. Katika hafla ya kukabidhi misaada hiyo, Bi Elvera ...

FANYENI UKAGUZI KWA WELEDI BILA YA KUMWONEA MCHIMBAJI YOYOTE – MHANDISI KAMANDO*

Image
_Wapendekeza maboresho Kanuni za Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira pamoja na Sheria ya Baruti._ 📍*Mwanza* WAKAGUZI wa Migodi ya Madini  na Baruti wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, kuongeza  ufanisi na kufuata  taratibu na sheria za nchi katika utoaji wa huduma. Hayo yamesemwa leo Mei 29, 2025 na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Hamisi  Kamando jijini Mwanza  wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha wakaguzi migodi na baruti ambacho kililenga kujengeana uwezo ikiwemo kufanya maboresho ya  Kanuni mbalimbali za madini na Sheria ya Baruti. ‘’Tusikubali kuyumba au kuyumbishwa na hatimaye kutolewa kwenye mstari, tuendelee kufuata misingi, weledi na maadili katika utendaji kazi kwa kuepuka rushwa na kushinda vishawishi   na tamaa nyinginezo,’’amesema Mhandisi Kamando na kuongeza, “Nitoe rai, tunatakiwa kuwajibika kwa kuzingatia nidhamu, uaminifu, uwazi na kuongeza bidii kwenye kazi katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madin...