RUAHA YAFANYA KIKAO NA WADAU WA UTALII KUELEKEA MSIMU MPYA WA UTALII - IRINGA.*


Na. Jacob Kasiri - Iringa.

Katika kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa utalii (high season) Juni, 2025, Hifadhi ya Taifa Ruaha imeendesha kikao maalumu kilichowakutanisha wadau wa utalii ili kujadili  Masuala mbalimbali kuhusu shughuli za Utalii,changamoto na mikakati ili kukuza utalii ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa Ruaha. 

Kikao hicho cha siku moja kilichofanyika jana Mei 30, 2025 katika Ukumbi wa Sunset Hotel mjini Iringa kimewajumuisha TANAPA, Mawakala wa Utalii, waongoza watalii (Guides), Mawakala wa Usafirishaji, wamiliki wa hoteli, wawakilishi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wizara ya Maliasili na Utalii-Kusini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Uhamiaji na Polisi.

Akielezea umuhimu wa kikao hicho Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Abel Mtui alisema,  “Wadau wote waliojumuika katika kikao hicho ni muhimu katika mnyororo mzima wa utalii ili kufikia maazimio ya pamoja katika kukuza sekta ya utalii Nyanda za juu Kusini na Tanzania kwa ujumla.


Aidha, Kamishna Mtui aliwaeleza washiriki wa kikao hicho mipango na mikakati mbalimbali ambayo hifadhi imejiandaa kuitekeleza kuhakikisha watalii wanapata huduma bora kulingana na thamani ya fedha zao, na alisisitizi kufanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na wadau hao.

Hifadhi ya Taifa Ruaha ni miongoni mwa Hifadhi za Taifa 21 zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambayo inapatikana katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Mbeya ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 19,822 ikisifika kwa kuwa na idadi kubwa ya Simba barani Afrika.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO