HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUSAIDIA KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA


Dodoma

Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara (Samia Infrastructure Bond) inaenda kuondoa changamoto ya kutokamilika kwa wakati  kwa ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara kutokana na ucheleweshaji wa malipo kwa makandarasi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA), Bi. Catherine Sungura wakati akijibu katika kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Alisema katika bondi hiyo, TARURA kwa kushirikiana na Benki ya CRDB imefanikiwa kukusanya bilioni 323 ambazo zitaenda kutumika kuwakopesha Makandarasi wazawa ili waweze kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Bi. Sungura alisema TARURA itaendelea kushirikiana na maafisa habari kwenye Halmashauri katika kutangaza kazi kubwa ya ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara nchini.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO